ASEMA INAKABILIWA NA UKAME WA VIONGOZI WALIOPIKIKA
KIMAADILI.
Hata
kupata wagombea hutegemea 'iokoteze' walioshindwa michujo au chaguzi za CCM. Asena
kwa mtaji huo haiwezi kuwa chama chenye tija na hatma njema kwa taifa.
KATIBU
Mkuu wa CCM, Wilson Mukama amesema Chadema hakiwezi kuwa chama chenye tija na
hatma njema kwa taifa kutokana na kulazimika kuokoteza hata wagombea wake
kutokana na wanaoshindwa kwenye michujo au chaguzi ndani ya CCM. Alisema,
Chadema na vyama vingine vya upinzania hapa nchini, vinazama katika hali hiyo,
kutokana na kutokuwa na tanuru imara linalowawezesha kutoa viongozi waliopikika
kimaadili, kama ilivyo ndani ya CCM. Amesema, Chadema wanaposema, kwamba kwa
CCM kutowafukuza au kuwanyima uongozi baadhi ya wana-CCM ni kuizika CCM, huko
ni kulia kinyume kwamba kwa kutofanya hivyo CCM imewakosesha watu ambao
wangehamia kwao hivyo chama chao kinakufa.
Mukama
alisema hayo jana wakati wa sherehe ya kuwapongeza wana-CCM Kata ya Msasani kwa
kukamilisha chaguzi zao ndani ya chama katika kata hiyo, iliyofanyika kweny6e
ukumbi wa Maisha Club, Msasani jijini Dar es Salaam. Mukama alisema, CCM ni
taasisi iliyojengwa katika misingi imara na mshikamano wake ni kama ngumi
inayoundwa na vidole vitano na kitaendelea kuwa imara kwa sababu viongozi wake
wanatokana na tanuru lililowapika kimaadili wakapikika.
"CCM
bwana ni tasisi yenye viongozi wenye chimbuko la maadili, siyo kama vyama
vingine vinaongozwa na wenye vilabu vya usiku halafu eti navyo ni vyama vya
kuweza kuongoza nchi", alisema Mukama. Alisema kutokana na CCM kuwa chama
chenye chimbuko la maadili bora, ndiyo sababu kila kinapofanya uchaguzi wa
kupata viongozi wake huwa ni wa kihistoria kwa kuwa anayepenya kuwa kiongozi
huwa amepita kwenye tanuru la uchujwaji wa hali ya juu.
"Juzijuzi
tulipokuwa tunateua majina ya wagombea, Kamati yetu ya maadili, haikuacha
kuchunguza hatua kwa hatua na kwa makini kama kila aliyeomba uongozi anazo sifa
bora na zinakidhi viwango vya kushinda anayetakiwa kuondolewa yeye abaki, hivi
ndivyo chama chenye misingi ya uadilifu ya uongozi kinavyokuwa", alisema
Mukama na kuongeza:- "Sasa hivi vyama vingine vinaweza kufanya mchujo wa
aina hii? thubutu.
Si
mlisikia juzi juzi mbunge mmoja alijaribu kuonyesha nia ya kutaka uenyekiti wa
Chama fulani, wee mliona alivyofurumushwa". Mukama alisema, wanaosema CCM
inakufa ni wavivu kufanya tathmini au wanasema hivyo kudanganya watu na nafsi zao
huku wenyewe wakiwa wanajua kwamba CCM ni imara tena kwa vigezo.
"Hivi
jamani tujiulize na wao (wapinzani) wakitaka pia wajiulize chama chenye
mwelekeo wa kufa kinaweza kupata wagombea ambao ni Wazee, Vijana kina baba na
kina mama tena wengi wasomi kabisa waliobobea hadi ngazi za uprofesa,
wanaokanyagana kwa wingi kama tulivyoona wakiomba uongozi katika nafasi
mbalimbali? ", alihoji Mukama. Alisema, tutokana na hali ya uchaguzi ndani
ya Chama iliyojionyesha katika ngazi za mikoa, baada ya kumalizika ngazi ya
taifa, CCM itakuwa itakuwa imara zaidi tayari kwa kutwaa dola tena baada ya
uchaguzi mkuu wa 2015.
Katika
hafla hiyo, wanachama wa Kata hiyo, waliuopongeza uongozi wa juu wa CCM kwa
namna ulivyoweza kuweka taratibu zilizo wazi na za haki katika kuhakikisha
uchaguzi ndani ya chama unazaa viongozi walio dhabiti. Mapema, Mukama
alikabidhi hati kwa vijanan na makamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM, ambao
wameshiriki katika shughuli mbali mbali za kuimarisha chama kwa namna moja au
nyingine.
No comments:
Post a Comment