To Chat with me click here

Friday, October 19, 2012

MTOTO JULIANA BARAKA ZAZIDI KUMSHUKIA


Afya ya mtoto  Juliana Mwinuka (16) mkazi  wa kitongoji cha Ushindi kata ya Mavanga  wilaya ya  Ludewa  mkoa  wa Njombe  imeendelea  kuleta matumaini baada ya kuanza kukaa mwennyewe  huku akiweza kuinua mikono yake jambo ambalo  linazidi  kutia matumaini  zaidi.

Taarifa mpya ya leo, kuna msamaria mwema kutoka nchini Marekani ameahidi kusaidia kumtafutia hospitali nchini Marekani mtoto Juliana iwapo hapa nchini itashindikana. 

Hata  hivyo bibi wa mtoto  huyo jana  kwa mara ya kwanza ameweza kusimulia udani halisi  wa tukio  hilo na kuwa si kwamba mtoto  huyo aliungua zaidi ya  miezi saba kama alivyodai awali alipozungumza na msamaria mwema  wa kwanza aliyepata  kuleta taarifa  hizi awali bali aliungua toka mwaka 2008 akiwa darasa la 4 na kuwa mtoto huyo baba hana ila mama yake yupo mzima japo ana matatizo ya akili 

Mtandao  huu  (Maxmillian Kattikiro Blog) unapenda  kushukuru jitihada mbali mbali  zinazoendelea  kufanywa na mitandao  mbali mbali ya kijamii kama Blog ,Facebook na Radio mbali mbali katika  kutoa taarifa  za mtoto  Juliana  pia kulishukuru gazeti la Amani la Leo kwa taarifa  yake juu ya mtoto Juliana Mwinuka .

Sababu  kuu ya kumhamisha  leo  kutoka Hospitali ya Muhimbili  kurudi tena CCBRT  ni  kutokana na kuwepo kwa taarifa  kuwa kuna madaktari bingwa kutoka nchi mbali mbali duniani watafika hapo kwa ajili ya  kuwafanyia matibabu  wagonjwa  waliopo hapo hivyo mtandao  huu kwa kushirikiana na wadau mbali  ambao wameendelea kumtakia afya njema mtoto  Juliana  tumefanya jitihada za kumwamisha na kumpeleka hapo ili kukutana na bahati  hiyo.

Mtandao huu unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu, mtoto Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi ni za mmiliki wa mtandao wa Francis Godwin anayeratibu shughuli zote za kuchangisha na matibabu ya mtoto Juliana.

Nawaomba tuungane kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto Juliana Mwinuka na Mungu atatuongezea zaidi

No comments:

Post a Comment