VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) wamenusurika kutekwa baada ya gari lao aina ya Toyota Opa
lenye namba za usajili T 850 BLK, kushambuliwa na watu wasiojulikana na
kuvunjwa kioo cha nyuma na kitu kizito.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 9, mwaka
huu majira ya saa nne usiku wakati viongozi hao wakitoka katika mkutano wa
uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani katika Kata ya Mpwapwa Mjini.
Shambulizi dhidi ya viongozi hao
waliokuwa katika gari hilo mali ya Eva Mpagama ambaye ni Mratibu wa Vijana
CHADEMA Mkoa wa Dodoma, lilifanyika katika eneo la Mwanakianga, nje kidogo ya
mji wa Mpwapwa.
Walioshambuliwa ni Mkurugenzi wa
Oganaizesheni na Mafunzo CHADEMA Taifa, Benson Kigaila, Mratibu wa Vijana Mkoa
wa Dodoma, Mpagama na Kunti Yusufu ambaye ni mratibu wa akina mama CHADEMA
mkoa.
Tukio hilo liliripotiwa Oktoba 10
katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Mpwapwa, na kufunguliwa jalada namba
RB/1934/2012.
No comments:
Post a Comment