To Chat with me click here

Thursday, October 11, 2012

UCHAGUZI WA CCM! WAGOMBE KUANGUKA NA KUPOTEZA FAHAMU

 Vailet Elias Sambilwa wakati akirudisha fomu ya kuwania Ujumbe wa NEC kupitia UVCCM.


WIMBI la wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi wa Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ kuanguka na kupoteza fahamu linazidi kushika kasi kufuatia hivi karibuni mgombea wa Ujumbe wa Halmashauri Kuu Taifa na Baraza Kuu UV-CCM, Vailet Elias Sambilwa naye kuanguka kisha kupoteza fahamu kwa saa kadhaa.

Kwa mujibu wa chanzo, Vailet (pichani) alikumbwa na mkasa huo, Oktoba 5, mwaka huu ndani ya Chuo cha Elimu ya Biashara ‘CBE’, jijini Dar es Salaam ambako anasomea uhasibu akiwa mwaka wa pili
Tulimsaka Vailet ili kutaka kujua kilichompata, alipopatikana alijibu kwa mkato kwamba hajui nini kilimtokea lakini alikiri.

“Yeah, ni kweli lakini sijui nini kilinitokea, lakini sidhani kama kuna umuhimu wa wewe kuniuliza kuhusu hilo, asante,” alisema Vailet na kukata simu.

Hivi karibuni, mgombea wa ujumbe wa NEC-CCM Wilaya ya Uvinza, Asha Baraka naye alipiga mwereka hatimaye kupoteza fahamu wakati matokeo ya uchaguzi huo yakiwa yanasubiriwa kwa hamu kubwa na wagombea. Uchaguzi aliojitosa Vailet unatarajiwa kufanyika Oktoba 20 na 21, mwaka huu mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment