NI JK, MKAPA, KINANA, MEMBE NA NAPE
VIGOGO
watano wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wako nchini Marekani, vyanzo vya habari
hii limebaini. Uwepo
wa vigogo hao Marekani kwa wakati mmoja, umeibua gumzo nchini hususan kwa
mitandao ya makada wa chama hicho wanaotajwa kutaka kuwania urais mwaka 2015.
Vigogo
hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, na mjumbe
wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC), Abdulhaman Kinana, ambaye amepata
kuwa kampeni meneja wa marais hao wawili.
Mwingine
ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, ambaye
amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa makada watakaowania urais mwaka 2015.
Wakati
vigogo hao wako nchini Marekani, kigogo mwingine wa CCM, Nape Nnauye, ambaye ni
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, anatarajia kwenda nchini Marekani
kesho.
Ingawa
vigogo hao wako Marekani kwa shughuli na sababu tofauti, mahasimu wa Waziri
Membe kisiasa wamehusisha ziara hiyo ya wazito hao na harakati za urais 2015.
Rais
Kikwete yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi. Rais na ujumbe wake uliondoka
nchini juzi na atakuwa hapo kwa siku mbili kabla ya kuelekea nchini Canada kwa
ziara nyingine rasmi ya kiserikali.
Habari
zinasema kuwa Mkapa na Kinana waliondoka nchini wakati vikao vya mchujo vya CCM
vikiendelea mjini Dodoma na wako nchini humo kwa ajili ya shughuli za taasisi
ya Mkapa Foundation na Nape anatarajia kwenda kwa shughuli zake binafsi.
Hadi
sasa hakuna kada yeyote wa CCM aliyetangaza kuwania urais, lakini mbali ya
Membe, duru za kisiasa zinawataja makada wengine wanaotaka urais kuwa ni pamoja
na mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa.
Hata
hivyo, kasi ya Sumaye kuwania nafasi hiyo imepunguzwa na matokeo ya uchaguzi wa
NEC, wilayani Hanang’ ambapo aliangushwa na Dk. Mary Nagu.
Wengine ni Samuel Sitta,
Dk. Abdallah Kigoda, Dk. Emmanuel Nchimbi, Dk. Asha Rose Migiro na wengine.
No comments:
Post a Comment