To Chat with me click here

Monday, October 15, 2012

MATUKIO MBALIMBALI HAPO JANA.

MWENGE WA UHURU

Rais Jakaya Kikwete akishikillia mwenge wa uhuru baada ya kuupokea kutoka kwa kiongozi wa mbio za Mwenge, Honest Mwanossa mjini Shinyanga jana, wakati wa kilele cha maadhimisho ya mbio za mwenge wa uhuru kumbukumbu ya miaka 13 ya kifo cha baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA
  
Watoa mada wa kongamano la maadhimisho ya miaka 13 ya kifo cha Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere kutoka kushoto ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Visensia Shule, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, Mwanasheria wa Kujitegemea, Esta Wassira na Meya wa Ilala, Jerry Silaa wakiwa kwenye maadhimisho hayo Dar es Salaam, jana.

  NASHUKURU KWA MSAADA

Mhariri wa Habari wa gazeti la MCL, Kizito Noya akimkabidhi Roida Mhema Sh1milioni  zilizotolewa na msamaria mwema ambaye hakutaka kutaja  jina lake kwa ajili aya matibabu ya Elbenezer Maulid ambaye ni mtoto wake anayeumwa kansa ya ngozi.

No comments:

Post a Comment