Kattikiro Jr. |
Leo Tarehe 2, Octoba ni siku ya kuzaliwa kwa Mpambanaji na Mwanahabari ambaye pia ni mmiliki wa Maxmillian Kattikiro Blog. Ndugu Kattikiro Jr. alizaliwa miaka kadhaa iliyopita, na leo amekuwa akitimiza miaka (guess ....) tangu siku hiyo ya kuzaliwa kwakwe.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, alieleza kuwa,
"Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake tele katika maisha yangu hadi leo nasherehekea siku nyingine ya kuzaliwa kwangu kwa zaidi ya mara 30. Sina cha kulipia wema huu wa Mungu zaidi ya shukurani kwakwe".
"Najua wengi walitamani kufikia hata nusu ya miaka yangu leo, lakini hawakupata fursa hiyo, hivyo umri huu au maisha haya ni zawadi toka kwa Mungu, hivyo nadhani ni vyema sana kuheshimu uahi wa kila mmoja na kuulinda kwa hali na mali. Huwa nachukizwa sana na ukatili unaofanywa na watu mbalimbali katika dunia hii, hususani hapa nchini, mfano: wakina mama wanaotoa mimba, kutupa watoto wachanga ambao hawana hata namna ya kujitetea, ukatili wa kijangili pamoja na kutowatendea haki kwa namna yeyote ile viumbe ambao hawana hatia."
"Hivyo naendelea kumshukuru Mungu hata kwa mafanikio madogo ya kimaisha aliyonipatia, pamoja na pumzi ambayo ameendelea kunijaalia kuwa nayo. Pia naomba wadau mbalimbali na wasomaji wa blog hii kuungana nami katika siku yangu hii muhimu, na kuniombea ili kuweza kusheherekea siku nyingine kama hii mwaka kesho".
Nawapenda wote !!!.
No comments:
Post a Comment