To Chat with me click here

Friday, October 5, 2012

TUENDELEE KUMSAIDIA MTOTO JULIANA MWINUKA, BADO ANAHITAJI MISAADA YETU KWA HALI NA MALI



Afya ya mtoto Juliana Mwinuka mkazi wa kijiji Cha Mavanga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi, hali ya afya yake ni mbaya kwa sasa, kula pamoja kunywa anatumia mipira maalum. 

Hata hivyo inadaiwa kuwa jitihada zinazofanywa na madaktari na wauguzi wa Hospitali hiyo ya Muhimbili kwa mtoto Juliana ni kubwa sana ambazo zinatia moyo kwa wauguzi wa mtoto huyo waliopo hapo. 

Hawa ni wadau waliojitokeza kuchangia kwa siku mbili hizi ni pamoja na; Msamaria asiyetaka kutajwa jina (Tshs. 10,000), Moses Nyirenda (Tshs. 35,000)Yvone Msechu (Tshs.50,000), Luiham Ringo (Tshs11,000), Gudila T. Mtalo (Tshs. 10,000) Peter Kerret (20,000), Beatha Kiwelo (5,000) na Godfrey Mwenesy (20,000). Wengine ni Frank Mchomvu (Tsh 11,000) na Atuboneksye Massapa (Tsh.20,000.  

Mtandao huu Maxmillian Kattikiro unaendelea kuwapongeza wote wanaoendelea kuguswa na kuungana na wadau wengine kumchangia fedha za matibabu, mtoto Juliana kama anavyoonekana akiwa ameunga uso wake kwa moto ni yatima anahitaji msaada wako ili kunusuru maisha yake waweza kutuma mchango wako kwa njia ya M-PESA katika namba hii 0754 026 299 au Tigo Pesa 0712 750199 namba hizi ni za mmiliki wa mtandao wa Francis Godwin.
 
Nawaomba tuungane kufanikisha kuokoa maisha ya mtoto Juliana Mwinuka na Mungu atatuongezea zaidi

NB. 
Mtoto  Juliana ni yatima na amekuwa akiishi na bibi yake na muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa  kifafa  hivyo siku alipokuwa peke yake jikoni ndipo alipoangukia katika moto na kuungua  hivyo na baada ya tatizo alikaa nyumbani kwa zaidi ya miezi saba sasa  bila matibabu na ndipo mtandao wa Francis Godwin ulipopata habari yake na kuendesha harambee  hii inayoendelea na msamaria mwema mmoja kujitokeza kumsafirisha hadi Dar ambako anapatiwa matibabu kwa  sasa.

No comments:

Post a Comment