To Chat with me click here

Friday, October 12, 2012

MDAHALO WA AZAKI ZA KIRAIA KESHO NI JIMBO LA IRINGA MJINI


Mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (chadema) kesho kushiriki  mdahalo na   wapiga kura  wake  jimboni kwake Iringa  katika mwendelezo wa midahalo ya kutathimini haki na fursa sawa kwa jinsi zote majimboni mwao.
Katika mdahalo huo ulioandaliwa na mtandao  wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika mkoa wa Iringa(ICISO -UMBRELLA) kwa kushirikiana na mitandao ya AZAKI  ya halmashauri ya manispaa ya Iringa (IMUCISO) na Iringa Vijijini (IRUNGO) mbunge Msigwa  ambaye ni mbunge wa  jimbo la  amealikwa  kushiriki mdahalo  huo ambao pia unaweza  kumshirikisha na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM)

Katibu mtendaji wa ICISO-UMBRELLA Raphael Mtitu alisema kuwa tayari mdahalo huo umefanyika katika jimbo la Kilolo ,Isimani  na Kalenga  .


Mititu alisema mbali  na majimbo hayo mdahalo  huo utahitimisha  kesho katika ukumbi wa VEta mjini Iringa  kwa kumshirikisha mbunge Msigwa .
Alisema kuwa   lengo la mdahalo huo ni kuongeza uewelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa haki na fursa sawa kwa jinsia katika mkoa wa iringa na wilaya zake kwa ujumla."lengo ni kuwapa wanajamii uelewa juu ya haki za kijinsia na kupunguza matukio ya ubaguzi na unyanyasaji wa kijinsia katika ngazi mbalimbali katika kaya,familia na jamii.

No comments:

Post a Comment