MWENYEWE ASEMA WANANCHI WA
MONDULI NDIYO MSULI WAKE
Mawaziri Wakuu Wastaafu, Fredrick Sumaye na Edward Lowassa wakiteta Jambo. |
SIKU
chache baada ya Waziri Mkuu mstaafu, Fredereck Sumaye, kubwagwa kwenye
kinyang’anyiro cha ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya
Hanang’ mkoani Arusha mwanasiasa huyo sasa ametangaza vita na Waziri Mkuu
mwenzake mstaafu, Edward Lowassa.
Sumaye
ambaye hajatangaza rasmi kuwania kiti hicho, anatarajiwa kupasua jibu wakati
wowote kuanzia leo kueleza kilichotokea; msimamo wake na kwamba yuko tayari
kuwania urais mwaka 2015 endapo Lowassa atawania kiti hicho.
Sumaye
aliangushwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji,
Dk. Mary Nagu, katika kuwania nafasi ya ujumbe wa NEC wilaya ya Hanang, matokeo
ambayo anaamini yana mkono wa Lowassa.
Chanzo
cha karibu na Sumaye, kilisema kuwa pamoja na Waziri Mkuu huyo mstaafu
kushindwa na Dk. Nagu kwa zaidi ya kura 167, amepokea matokeo hayo kwa shingo
upande kwa kile alichoeleza kuwa ushindi huo ni wa mafisadi.
“Hataki
kuzungumza chochote leo ila atazungumza nanyi wakati wowote kuanzia leo, lakini
anasema ikiwa Lowassa atawania urais, Sumaye ataingia katika mpambano huo
kukabiliana naye kwa njia yoyote. Hataki kusema ataingia kwa CCM au chama gani
au mgombea binafsi,” anaeleza mtu wa karibu na Sumaye.
Mbali
ya kundi la Sumaye na wanasiasa wengine kuanza mkakati huo, wapo pia wanasiasa
wengine wenye majina makubwa ndani ya chama, serikali na wastaafu wanaotajwa
kuingia kwenye muungano huo.
Akijibu
tuhuma hizo kwa kifupi, Lowassa alisema endapo Sumaye ataitisha mkutano na
waandishi wa habari na kutoa tuhuma hizo, nitajibu.
Hata
hivyo, baadhi ya wafuasi wa Sumaye na watendaji wa ndani ya serikali wamesema
kuanguka kwa mwanasiasa huyo mkongwe katika uchaguzi wa wilaya kunamuweka
vizuri zaidi kisiasa kutokana na mazingira tete ya kisiasa ndani ya CCM, chama
ambacho kimechokwa na umma.
Waziri
wa zamani wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) na mbunge wa zamani wa jimbo la
Makete, Dk. Hassy Kitine, alikaririwa juzi akisema kuwa kuangushwa kwa Sumaye
katika nafasi ya NEC hakuwezi kumuathiri kisiasa kama atachukua uamuzi wa
kuwania urais mwaka 2015 kupitia CCM.
Dk.
Kitine alitoa kauli hiyo alipoombwa na gazeti moja kutoa maoni yake juu ya
matokeo ya NEC wilayani Hanang’ kama yana athari kwa mustakabali wa kisiasa kwa
kiongozi huyo.
“Katiba
ya CCM haina kipengele kinachosema kama unataka kuwania urais ni lazima uwe
mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM , kwa hiyo nasema kama kweli Sumaye anatafuta
urais bado ana nafasi ya kuwania nafasi hiyo,” alikaririwa akisema Dk. Kitine.
Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, naye alimtia moyo Sumaye kwa
kuweka bayana kuwa uchaguzi wa NEC ni wa ngazi ya wilaya tu kwa hiyo Sumaye
anaweza kuwa anakubalika kitaifa kuliko katika wilaya anayotoka huku akitumia
usemi kwamba ‘nabii hakubaliki kwao’.
Katika
hatua nyingine, hali inaelezwa kuwa tete ndani ya CCM baada ya kuwapo kwa
taarifa za ushangiliaji kutoka kwa wafuasi na viongozi wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) ambao wameona wanazidi kusafishiwa njia.
“CHADEMA
wameshangilia sana kwa kuwa sasa jimbo hilo litachukuliwa kirahisi. Walikuwa
wanamuogopa Sumaye na kumheshimu hivyo kwa sasa watu wake wote wanahamia
CHADEMA.
“Wanasema
mafisadi walihakikisha wanampa kila mjumbe kiwango cha chini kabisa cha
shilingi 100,000 kumuangusha Sumaye. Uongozi wote wa CCM wa wilaya na hata
baadhi kwenye mkoa walijipanga kumuangusha,” anasema.
Katika
uchaguzi huo wa Hanang, hali ilianza kuwa tete toka hatua za awali, ambapo Dk.
Nagu alitajwa kushinikiza kubadilishwa kwa muhtasari wa kikao cha wilaya
kilichokata jina lake na hivyo kurudishwa tena.
Taarifa
kutoka Hanang zinaeleza kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU), ilifanya kazi katika mazingira ya aibu kutokana na kuonekana
kufumbia macho vitendo vya rushwa iliyogawiwa waziwazi.
Hivi
karibuni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah, alinukuliwa akisema
kwamba taasisi yake inafuatilia kwa karibu uchaguzi huo ndani ya CCM ili
kubaini watu wanaotumia rushwa, kauli ambayo imeelezwa kuwa ya kisiasa zaidi.
Dk.
Hoseah alitoa kauli hiyo akijibu hoja mbalimbali za washiriki wa kongamano la
kujadili utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa kupambana na rushwa nchini
na mapendekezo yanayopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa mpango wa awamu ya
tatu (2012 – 2016).
Uchaguzi
huo ulifanyika siku chache baada ya CCM kupitisha majina ya walioomba nafasi
hizo huku wanachama wengi wakienguliwa kutokana na kukosa sifa katika kikao
kilichomalizika mjini Dodoma mapema wiki hii.
Katika
hatua nyingine, Lowassa ametamba kuwa wananchi wa Monduli ndiyo msuli wake wa
kisiasa. Akizungumza
baada ya ushindi wa NEC alioupata, Lowassa alisema ushindi huo mkubwa
umedhihirisha kuwa ana misuli ya kisiasa kwa wananchi wake.
“Kuna
mzee rafiki yangu aliniambia kuwa katika kazi za siasa angalia ‘grass roots’,
watu wanakuwa ndiyo msuli wako kisiasa, na mimi watu wa Monduli ndiyo msuli
wangu,” alisema Lowassa ambaye anatajwa kuwa mmoja wa watu watakaowania urais
mwaka 2015.
“Wananchi
wa Monduli mmenithibitishia hilo na nawashukuru sana kutoka kwenye sakafu ya
moyo wangu, jibu la thibitisho hilo kwangu ni utumishi uliotukuka kwenu,”
aliongeza.
No comments:
Post a Comment