Climate Change Advisor at United Nations Development Programme, Dr Amani Ngusaru |
Mshauri mkuu wa mabadiliko ya hali ya
hewa katika Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) Amani Ngusaru aliwataka
Watanzania wanaoishi karibu na Msitu wa Pugu kukumbatia mfumo endelevu wa
maisha.
"Mnazo changamoto nyingi zikiwemo
kuongezeka kwa uchafuzi wa hali ya hewa, na katika suala hili, maendeleo
endelevu ni muhimu na kila mtu analazimika kuyalinda mazingira," Ngusaru
alisema, kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la Tanzania.
Msitu wa Pugu ni moja ya mfumo wa
ikolojia mkongwe kabisa ulimwenguni, ambao ni makazi ya aina 80 za ndege na
maji safi ya Mto Msimbazi ambayo yanatoa maji ya kunywa kwa jamii za jirani,
alisema, na kuongeza kuwa unahitajika kulindwa kutokana na athari hasi za
mabadiliko ya hali ya hewa, kama vile upungufu wa maji, umalizaji wa mfumo wa
ikolojia, upatikanaji duni wa nishati na kuenea kwa jangwa.
Ngusaru aliwataka Watanzania kuangalia
katika matumizi ya vyanzo vya nishati mbadala na majiko ya kupikia ya kuokoa
nishati ili kusaidia juhudi za serikali za kupunguza athari za mabadiliko ya
hali ya hewa na kuboresha shughuli za maendeleo endelevu.
No comments:
Post a Comment