Pembe za ndovu zilizokamatwa katika operesheni dhidi ya biashara ya magendo huko Hong Kong zikioneshwa kwenye mkutano wa vyombo vya habari hapo tarehe 20 Oktoba. |
************************************
Viongozi
wa Tanzania wakataa kuhusika na tani 3.18 pembe za ndovu za magendo
zilizokamatwa huko Hong Kong mwishoni mwa wiki, wakidai kuwa idadi kubwa kama
hiyo ya pembe za ndovu haiwezekani kuwa zimetoka nchini kwao, gazeti la Daily
News la Tanzania liliripoti siku ya Jumatatu (tarehe 22 Oktoba).
Viongozi
wa Hong Kong walisema kuwa pembe hizo zilikuwa zimesafirishwa kutoka Kenya na
Tanzania na zilikuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 3.4
"Tanzania
imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuwia uwindaji haramu wa tembo na wanyama
wengine wa msituni," alisema Paul Sarakikya, afisa wa wanyamapori katika
Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania. "Inaweza kutokea kwa kesi adimu
sana, lakini kiwango kikubwa kama hicho cha pembe za ndovu haziwezi kuwa
zimekusanywa kutoka nchini."
Sarakikya
alisema kuwa wawindaji haramu wanaofanya kazi hiyo katika nchi zisizo bahari
kama vile Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo au Mozambiki hutumia bandari
ya Dar es Salaam kusafirisha bidhaa zao, na kuongeza kuwa bandari inapaswa
kufanya upekuzi zaidi wa makontena yanayotoka nje ili kuzuwia biashara haramu
ya pembe za ndovu.
Hivi
karibuni Tanzania iliomba idhini kutoka kwa Makubaliano ya Kimataifa juu ya
Biashara ya Kimataifa ya Wanyama Walio Hatarini ili kuuza baadhi ya lundiko la
pembe zake za ndovu, zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 87.8 (dola
milioni 55.5).
No comments:
Post a Comment