To Chat with me click here

Monday, October 8, 2012

DR. MWANJELWA ATOKA HOSPITALI BAADA YA AFYA YAKE KUIMARIKA.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Dr. Mary Mwanjelwa.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) kutokana na ajali mbaya aliyopata mkoani humo ameruhusiwa baada ya hali yake kuwa nzuri.

Dk. Mwanjelwa alipata ajali Jumanne ya wiki iliyopita ambayo ilisababisha vifo vya watu 11 ambapo yeye (Dk.Mwanjelwa) alijeruhiwa na kulazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini kabla ya kuhamishiwa MOI.

Ofisa Habari wa MOI, Jumaa Almas, akizungumza na NIPASHE jana alisema Dk. Mwanjelwa ameruhusiwa kutoka katika taasisi hiyo Ijumaa wiki iliyopita baada ya halri yake kuwa nzuri.

Hata hivyo gazeti hili ambalo lilifika juzi katika taasisi hiyo lilielezwa na madaktari waliokuwa zamu kuwa pamoja na kuruhusiwa mbunge huyo ataendelea kuihudhuria kliniki katika taasisi hiyo katika siku ambazo amepangiwa.

Jumanne ya wiki iliyopita kulitokea ajali iliyosababisha vifo vya watu 11 akiwemo katibu wa Dk. Mwanjelwa ambayo ilitokana na lori la mafuta lenye namba T 911 BUV na tela lake T  841  BTC  kuyagonga magari manne.

Lori hilo ambalo lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) lilisababisha ajali hiyo baada ya kufeli breki na kuyagonga magari hayo likiwemo gari la Dk.Mwanjelwa, basi dogo la abiria Toyota Hiace lenye namba  T 887 AHT na kusababisha vifo vya watu hao.

No comments:

Post a Comment