Sheikh Farid Hadi Ahmed |
Wasiwasi umetanda
kisiwani Zanzibar kufuatia kutoweka kwa kiongozi wa kidini Sheikh Farid Hadi
Ahmed.
Watu wawili wametiwa
nguvuni waliohusika na maandamano na ghasia zilizosababisha uharibifu mkubwa
kisiwani humo.
Kuna hofu kuwa kiongozi
huyo huenda amekamatwa na polisi na anazuiliwa Tanzania bara kutokana na kuwa
amepinga utawala wa chama tawala cha Tanzania bara CCM.
Kwingineko, hapo jana
polisi nchini Tanzania walimkamata mhubiri mwenye utata anayetuhumiwa kwa
kuchochea vurugu wiki jana, na kusababisha maandamano mapya.
Kulingana mkuu wa polisi,
Suleiman Kova, Sheikh Ponda Issa Ponda, mkuu wa Jumuiya ya waislamu, vuguvugu
ambalo halitambuliki na serikali ya Tanzania, alikamatwa kwa kuchochea vurugu.
Kukamatwa kwa Sheikh
Ponda, mini Dar es Salaam, inakuja baada ya kukamatwa kwa watu 31 waliozua
vurugu na kupora mali ya watu wakati waandamanaji walijawa na ghadhabu na
kuandamana wiki jana wakiharibu makanisa kadhaa mjini humo.
Maandamano ya wiki jana
yalisababishwa na tetesi kuwa kijana mwenye umri wa miaka kumi na miwili
aliikojolea Quran.
Ponda amekuwa akiwaongoza
wafuasi wake kufanya maandamano kinyume na sheria na kutoa wito wa ghasia na
umwagikaji damu mjini Dar es Salaam na nchini kote.
No comments:
Post a Comment