MBUNGE
wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), amewataka Watanzania kukichukulia Chama cha
Mapinduzi (CCM) na kukiona kama janga la kitaifa kwani kimeshindwa kutatua
matatizo yao.
Kauli
hiyo aliitoa juzi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani
katika kata ya Msalato, manispaa ya Dodoma.
Mnyika
alisena kuwa CCM imechangia kwa kiasi kikubwa kuwadidimiza Watanzania kutokana
na kushindwa kusimamaia rasilimali zilizopo na kuwaruhusu wageni kuzitumia bila
kuwashirikisha Watanzania.
Alisema
kuwa Watanzania wengi wamekuwa maskini katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru
wakati kuna wachache ambao wanamiliki fedha nyingi. CHADEMA
wamemsimamisha Nsubi Bukuku kuwa mgombea udiwani katika kata hiyo.
Naye
Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, alisema vurugu zilizotokea juzi kabla
ya mkutano wao juzi zilisababishwa na wanachama wa CCM kuvamia msafara wao.
Majeruhi
katika vurugu hizo ni Katibu wa UVCCM wa kata ya Kiwanja cha Ndege, Ali
Swalehe; mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa CCM Dodoma Mjini, Fatma Mwihidini;
Diwani wa kata ya Uhuru, Ali Kimaro; Hussein Mtengule na Waziri Shabani.
Hata
hivyo, habari hizo zilisema kuwa hakuna mtu anayeshikiliwa na polisi kuhusiana
tukio hilo hadi sasa. Kamanda wa polisi mkoani
hapa, Stephen Zelothe, alipoulizwa kuhusiana na vurugu hizo alisema yuko
safarini kurejea mjini Dodoma na kwamba angetoa taarifa kwa waandishi
atakapofika.
No comments:
Post a Comment