Serikali
yetu ni bingwa sana katika kuzungumza ila si katika utendaji huu ni
uwanja wa ndege wa muda sana hapa mkoani Iringa lakini
gari linalotumika kwa ajili ya kuzima uokoaji katika uwanja huo ni
kituko kama ambavyo unaona pichani .
Mbali
ya wizara hiyo ya uchukuzi kuendelea kubadilishwa mawaziri na
manaibu wake kila wakati ila hakuna jipya ambalo wamekuwa wakilifanya kwa
uwanja huu ambao ni tegemeo katika mkoa wa Iringa hasa ukizingatia kuwa
mawaziri hao, manaibu na viongozi wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya
wamekuwa wakibadilisha magari kila wakati huku wakisahau kuwa uwanja huo
ndio wao wamekuwa wakiutumia pindi wanapokuja Iringa sasa ikitokea
ajali ni wa kwanza kuunda tume za kuchunguza chanazo cha ajali.
Nini
maoni yako mdau wa mtanado huu juu ya uwanja huu wa Nduli
Iringa?
No comments:
Post a Comment