To Chat with me click here

Friday, October 5, 2012

MAANDALIZI MAZISHI YA KARDINAL RUGAMBWA YAMEKAMILIKA

1st African Cardinal, Laurian Rugambwa.
KANISA Katoliki Jimbo la Bukoba,liko mbioni kukamilisha kuhamisha masalia ya mwili wa marehemu Muadhama Kardinali Laurian Rugambwa. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba jana,Askofu Msaidizi Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini alisema shughuli za maandalizi ya kuhamisha masalia ya mwili wa marehemu Kardinali Rugambwa inaendelea vizuri.

Alisema mbali ya kukamilika kwa maandalizi hayo, ujenzi wa kanisa jipya uko hatua za mwisho kabisa kumalizika.

Alisema shughuli ya kuhamisha masalia ya mwili wa marehemu Kardinali Rugambwa, itafanyika Jumamosi ya wiki hii kutoka Kanisa la Mama Bikira Maria la Kashozi lililoko nje kidogo ya Manispaa ya Bukoba.

Alisema sherehe hizo, zitaambana na sherehe zingine mbili ambazo ni maadhimisho ya miaka 100 ya kuzaliwa marehemu Rugambwa na sherehe ya kutabaruku kanisa la Kiaskofu la Jimbo ambayo itafanyika Jumapili.

Alisema akiwa Askofu wa Jimbo la Bukoba,marehemu Rugambwa aliweza kuchangia maendeleo mbalimbali mkoani Kagera,mojawapo ikiwa kuchangia shule za msingi,sekondari ya Rugambwa,hospitali za Mugana na Kagondo.

“Na mimi najivunia kuhazimisha sherehe hizi, kwani mmojwapo ya watu waliofaidika na mhadhama Kardinali Rugambwa,kwani niliweza kupelekwa Roma kusoma kwa maamuzi yake,”alisema Askofu Kilaini.

Marehemu Rugambwa,anakumbukwa kuwa askofu wa kwanza Mtanzania na Kardinali wa kwanza barani Afrika.

Maadhimisho ya sherehe hizo, yanatarajiwa kuhudhuriwa wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi takribani 15,000, huku Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment