MAPOKEZI ya Kihistoria
katika jiji la Arusha yamefanyika leo wakati wafuasi, Mbunge wa Arusha
Mjini kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema
walipo miminika kwa Wingi kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(KIA) hadi katika Viwanja vya Kilombero mjini hapa alipohutumia maelfu ya wana
CHADEMA Arusha Mjini. SOMA ZAIDI:www.mrokim.blogspot.com
Mapokezi yahoo
yamefanyika wakati Godbless Lema alipokuwa akirejea mjini Arusha akitokea
jijini Dar es Salaam kusikiliza hukumu ya Rufani ya Keshi yake ya Kuvuliwa
Ubunge iliyotolewa maamuzi ya kumrejeshea Ubunge wake Desemba 21,2012.
Maelfu ya wananchi wakiwa
katika msafara mrefu zaidi ya pikipiki 500 na magari ulianzia Uwanja wa Ndege
KIA mara baada ya Mbunge huyo kuwasili uwanjanai hapo majira ya saa 4:20
Asubuhi.
Aidha Maandamano hayo ya
Mapokezi ya Mbunge huyo, hayakuwa na hata chembe ya Askari Polisi waliovalia
sare wala magari yao ya diria kama ilivyozoeleka na kuyafanya yafanyike kwa
amani na utulivu katika maeneo yote yaliyopita.
Huku wakiimba nyimbo za
furaha hasa zile za “Oya oya Jembe letu limerudi” Wanachadema hao walijigawa na
baadhi kulinda amani huku wengine wakiongoza magari.
Father Kidevu Blog
ilishuhudua maelfu ya wakazi wa mji wa Arusha wakiwa katika hali ya furaha na
kusimama kando ya barabara kushuhudia mapokezi ya Mbunge huyo.
“Haijawahji tokea hapa
Arusha, kuwapo kwa msafara mrefu namna hii wa mapokezi ya kiongozi yeyote Yule,
tena yakiwa na amani ya kiasi hiki,” alisikika akisema mmoja wa Watu
waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.
Licha ya Kufanya mapokezi
hayo na Kumshukuru Mungu kwa Mbunge wao kurejea madarakani, lakini Wakazi wa
Arusha na Wapigakura wa Godbless Lema wamesema hivi sasa Mbunge huyo anapaswa
kutulia na kutumia kipindi kilicho baki cha miaka miwili ya madaraka yake
kuwatumikia wananchi katika kuhakikisha miradi ya Maendeleo inafanyika Jimboni
humo na kuachana kabisa na migomo na maandamano ya kila mara.
“Sasa Lema anatakiwa
kututumikia wananchi maana sisi tumesha mtumikia yeye vya kutosha kwa kuwa nae
bega kwa bega katika kipindi chote cha uongozi na hata alipokumbwa na msukosuko
wa kuondolewa Ubunge, hivyo sasa ni wakati muafaka wa yeye kuwaletea maendelea
wana Arusha Mjini,” alisema Meshack Siriwa.
Godbless
Lema alivuliwa Ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5,
2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika
hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha yaliyo
wasilishwa na wanachama watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha
kutengua ushindi wa Mbunge huyo.
Mke wa Godbless Lema akiwa na mtoto wao ndani ya gari wakati wa mapokezi hayo |
Lema akiwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari |
No comments:
Post a Comment