To Chat with me click here
Showing posts with label Habari. Show all posts
Showing posts with label Habari. Show all posts

Monday, December 29, 2014

KAFULILA: ESCROW INAZAMISHA NCHI


Mbunge wa Kigoma Kusini(NCCR-Mageuzi),
David Kafulila.

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, amesema kashfa ya kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), itaendelea kutafuna uchumi na kuongeza umaskini nchini kutokana na serikali kusuasua kuchukua hatua kali dhidi ya wahusika.

Kafulila, ambaye ndiye mbunge aliyeibua mjadala kuhusu kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow, bungeni, alisema hayo alipokuwa akitoa tathmini ya kufunga mwaka 2014 jana.

Kutokana na hali hiyo, alisema wahisani hawatachangia bajeti ya mwaka huu na ya mwaka ujao na hivyo, kuiweka serikali katika wakati mgumu.

“Hii itaidhoofisha CCM na kuijenga Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) 2015 na hivyo, uchaguzi kuwa mgumu na wa kihistoria,” alisema Kafulila.

Alisema mwaka 2014 umemalizika Bunge likiwa limejijengea imani kubwa kwa wananchi, huku serikali ikiporomoka kutokana na namna Bunge lilivyosimamia sakata la akaunti hiyo na serikali ilivyosuasua kushughulikia.

Kafulila alisema hakuna matumaini ya kiuchumi katika mwaka ujao wa 2015 kwa sababu nchi itakuwa na mahitaji makubwa ya uchaguzi, vitambulisho vya taifa na kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa, mambo ambayo yatahitaji fedha nyingi, ambazo hakuna.

Alisema sababu mojawapo iliyochangia uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika Desemba 14, mwaka huu, kuharibika ni serikali kukosa fedha.

Kafulila alisema wakati kukiwa na mambo hayo makubwa yanayohitaji fedha, serikali mpaka sasa ipo taabani kifedha kiasi, ambacho hata kandarasi za barabara zimesimamishwa kutokana na ukata. 

Alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inakusanya Sh. bilioni 800 kwa mwezi wakati mahitaji ya mishahara peke yake ni takriban Sh. bilioni 500, hivyo zinabaki Sh. bilioni 300, ambazo hazitoshi hata kunulia karatasi na mafuta kuendesha ofisi za serikali nchini kote.

Kafulila alisema licha ya uchumi kukua, maendeleo hayaonekani kwa sababu unakuzwa na sekta za madini, utalii, mawasiliano, ambazo hazibebi watu wengi, pia kero ya maji, ambayo kwa mujibu a utafiti wa taasisi ya Synovate, ni kero namba moja Tanzania, lakini serikali imeshindwa kabisa, ingawa ipo kwenye nchi ya 11kwa mito mingi duniani.

“Bado tunakosa wawekezaji wa kimkakati kwa mfano wa uamuzi wa serikali kuchukua mkopo wa dola bilioni 10 kwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo wakati pesa hiyo ingetosha kujenga reli ya kati ya kimataifa kwa dola bilioni sita na ziada ya dola bilioni nne zingetosha kupanua na kuimarisha bandari ya dare s Salaam, Mtwara, Tanga,” alisema Kafulila.

Saturday, October 18, 2014

MWANASHERIA MKUU MPYA ZANZIBAR AAPISHWA!




Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein amemuapisha mwanasheria mkuu mpya wa Zanzibar Said Hassan Said akichukua nafasi ya Bw. Othman Masoud.

Hafla ya kumuapisha Bw. Said ilifanyika ikulu ya Zanzibar Jana (Friday , 17th Oct , 2014) na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa seriklai akiwemo makamu wa kwanza wa Rais Malim Seif Sharrif Hamad, Waziri wa Bishara Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Mazrui, mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibu Abdullah Mwinyi, Mufti mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Mstahiki Meya wa Zanzibar Mhe. Abdulrahman Khatibu na vingozi wengine wa serikali.

Uteuzi wa Bw Said Hasan Said ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa naibu mwanasheria mkuu imekuja baada ya Dr Ali Shein Rais wa Zanzibar kumfuta kazi mwanasheria mkuu wa Zanzibar Bw Othman Masoud Othman wiki iliyopita huku kukiwa hakuna sababau yeyote iliyotolewa na serikali.

Ingawa Duru za siasa zianoyesha wazi wazi kuwa kufutwa kwake kazi ni kutokana na kupinga baadhi ya vifungu vya Katiba Inayopendekezwa wakati wa upigaji kura na kabla ya hapo kujiondoa katika kamati ya uandishi wa Katiba hiyo.

Friday, May 16, 2014

WHO OWNS UDA?



Malima: DCC holds 51 pct, govt 49, Simon Group: We have 76 pct stake

Deputy Finance minister, Adam Malima
Deputy Finance minister, Adam Malima yesterday asserted that the government hasn't sold any of its shares in the Dar es Salaam Transport Company (UDA) to the Simon Group Company.

Malima gave the government’s stand when responding to a question raised by Kawe MP, Halima Mdee (Chadema) who sought government’s explanation on its shares in UDA.

Mdee also wanted to know the real owner of the Dar es Salaam transport firm and the distribution of shares.

Malima clarified that the Dar es Salaam City Council and the government through Treasury Registrar are the owners of the company.

Regarding the distribution of shares, the minister said: “Dar es Salaam City Council has 51 percent of shares in UDA while the government has 49 percent.”
He however said that in 2006 the government expressed intention to sell its shares in order to get a potential investor who would have the ability to improve UDA.

He said the Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) was tasked to spearhead the exercise, though the commission failed to find an investor who would meet the requirements.

The minister said in January 2010, the Board of UDA notified the government on the possibility of getting an investor—Simon Group Limited, who would have bought the government’s stake and 7,880,303 unclaimed shares.

“After receiving the recommendations, the government directed the UDA board not to continue with the plan of selling shares to the Simon Group Limited because the procedures and regulations of obtaining the investor were violated,” he said.

UDA was established in 1974 with authorised share capital of 1,500,000,000/- which is equivalent to 15,000,000 shares at the price of 100/- each. Of the total shares, 7,119,697 were paid up while 7,880,303 unfixed.

According to the minister, on October 1, 2000 the government gave DCC about 3,631,045 shares out of 7,119,697 (51 percent) and retained 3,488,651 (49 percent) of the paid-up shares.

Speaking to The Guardian over telephone interview yesterday, Simon Group Executive Chairman Robert Kisena, said Malima’s statement is misleading.

“I am on my way from Dodoma to Dar es Salaam but as far as I know Simon Group own 76 plus shares in UDA while the government owns 23-24 percent of the shares. Soon we are taking the remaining shares that the government owns. We are at an advanced stage,” he said.

According to the MD, it is surprising to hear the deputy minister informing the public that the government and Dar es Salaam City Council own the firm 100 percent.

The Simon Group directed this paper to cross check with the Business Registration and Licensing Authority on the actual shareholders or how many shares each owns.

SOURCE: THE GUARDIAN