To Chat with me click here

Monday, October 1, 2012

WASSIRA SASA AWASHA MOTO KWA DR. SLAA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Bw. Stephen Wassira, amesema watoto wa kaka yake ambao juzi walitangaza kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bi. Lilian na Bi. Esther Wassira, wana haki ya kujiunga na chama chochote cha siasa.

Alisema kitendo cha Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibrod  Slaa kutumia jina na cheo chake wakati akiwapa kadi wanachama hao ni upotoshaji unaofanywa na CHADEMA ili kujipatia umaarufu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Bunda, mkoani Mara, Bw. Wassira alimshukia Dkt. Slaa na kumtaka awe makini kuwaita wake za watu chumbani na kuwapa kadi bila maofisa wengine wa chama hicho kushuhudia tukio hilo.

“Namhadharisha Dkt. Slaa kwani alichokifanya kinaweza kuleta mtafaruku katika ndoa za watu, Lilian na Esther ni watoto wa kaka yangu George Wassira si mimi, hawa ni watu wazima na wote wana haki ya kuchagua chama wanachokitaka,” alisema.

Aliongeza kuwa, Dkt, Slaa anaishi kwa kutafuta matukio bila kutumia akili ambapo mume wa Bi. Lilian ni mwanachama wa CHADEMA hivyo uamuzi aliochukua mkewe hauna uhusiano wowote na ukoo wao.

“Hata Makongoro Nyerere awliwahi kujiunga NCCR-Magezui wakati hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (baba yake), akiwa hai, je, tatizo lilikuwa wapi na yeye ni mtu mzima,” alisema.

Alisema siku zote Dkt. Slaa na viongozi wengine wa CHADEMA wamekuwa wakichukizwa na jinsi anavyojibu hoja zao hivyo wanachokifanya ni kumtafutia tuhuma lakini wameshindwa kufanikiwa hivyo wamezna kuwachonganisha katika ukoo.

“Wanachukizwa ninavyojibu mambo yao hasa wanayosema katika majukwaa na kuhatarisha amani, mimi ni mzalendo wa kweli ambaye nalitumikia Taifa lengu kikamilifu na sina tuhuma za ufisadi ambao Dkt. Slaa ameufanya kuwa wimbo,” alisema.

Hata hivyo, aliwataka Watanzania waelewe kuwa ukoo wao msingi wake si vyama vya siasa bali kila mtu ana haki ya kuingia na kutoka katika chama chochote.

Alisema kitendo cha Dkt. Slaa kuhusisha ukoo huo na tukio la watoto hao kujiunga CHADEMA ni kuwadanganya Watanzania kuwa ukoo huo umegawanyika jambo ambalo si kweli.

Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa kadi walikuwa na haya ya kusema:Ester wasira: (Ni mwanasheria, graduate wa UDSM)

(i)    Chadema ni Chama cha kizalendo na mkombozi wa dhati wa Mtanzania. 

(ii)         Chadema kinaleta matumaini mapya kwa Watanzania hasa vijana wasio na kazi na matumaini, Watanzania wenye maisha magumu hata kushindwa kumudu milo miwili kwa siku, akina mama wanaohangaika vijijini bila matibabu ya uhakika, maji, umeme, nyumba bora nk 

(iii)         CCM imedumaza nchi, nchi imekuwa kama mtu aliyedumaa kwa kukosa protein, haikui tena, Chadema ni damu mpya yenye kuweza kuingiza protein kwenye mishipa ya nchi iweze kufufuka na kukua tena. 

(iv)          Chadema kina viongozi imara na kwa maneno na matendo yake wanawadhihirishia watanzania kuwa ni waadilifu na wana nia njema ya kuipeleka Tanzania mbele. Alimalizia kwa kuwaasa vijana, akina mama na wazee wajiunge na M4C ili kuijenga Tanzania mpya. Alimalizia kwa kusema, “Kwa msaada wa Mungu, Tanzania Mpya inakuja. 

Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO): (i) Alielezea furaha yake kwa kujiunga na Chama makini na chenye kuleta matumaini mapya kwa mtanzania 

(i)      Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia Chadema kura 

(ii)     Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua hatua ya kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala. Alisema hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania hawathubutu kuchagua chama mbadala na badala yake kuendelea kuichagua CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi 

(iii)    Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hivyo ni wakati sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo mapya na kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo. 

(v)             Anasema ana imani na sera za chadema kuwa ndizo zitatukomboa. Amewapa moyo viongozi wa Chadema wasitishwe na vitisho na mauaji yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo tayari kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama itambidi afanye hivyo.

(vi)           Kwamba Chadema ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu isipokuwa tu watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura. (vii) Nae alimalizia kwa kusema “Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya inakuja.”Dr Slaa alitiwa moyo sana na ujasiri ulioonyeshwa na vijana hawa pamoja na maneno ya kizalendo waliyoongea na akawakarisha kwenye uwanja wa mapambano ya M4C.

No comments:

Post a Comment