To Chat with me click here

Friday, August 10, 2012

WATU ZAIDI YA 15 WARIPOTIWA KUFARIKI DUNIA KATIKA AJALI DARAJA LA MTO WAMI LEO

Watu zaidi ya 15 wameripotiwa kufariki Dunia leo katika mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakitokea Nairobi, nchini Kenya kuja Dar-es-Salaam leo. Ajali hiyo inaelezwa kuwa imetokea katika daraja la mto wami mkoani Pwani alfajiri ya leo. 

Mabasi hayo yanaaminika kuwa yalikuwa yamebeba waimbaji wa injili, waliokuwa wanakuja mjini Dar-es-Salaam katika kongamano ambalo lilitakiwa kufanyika mjini hapa hivi karibuni katika viwanja vya Jangwani. 

Baadhi ya majeruhi na marehemu katika ajali hiyo waliletwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kutibiwa na kuhifadhi miili hiyo.



Magari ya kubebea wagonjwa "Ambulance" yakiwa yamepaki mbele ya Jengo la emergency la hospitali ya Taifa Muhimbili huku yakishusha majeruhi katika ajali hiyo. 
Lori lililokuwa limebeba baadhi ya miili ya merehemu wa ajali hiyo, nalo likiwa limepaki mbele ya majengo hayo ya emergency baada ya kuwasili hospitalini hapo likitokea eneo la ajali, wami mkoani Pwani.
Gari la Jeshi la polisi toka katika ofisi ya RPC mkoa wa Pwani likiwa limebeba mizigo ya waliokuwa abiria wa mabasi hayo katika kuhakikisha usalama wa mizigo hiyo ya abiria baada ya kutokea kwa ajali hiyo. 
Baadhi ya majeruhi waliopokelewa katika hospitali hiyo toka kwenye magari ya kubeba wagonjwa wakitokea katika eneo la ajali mto wami, mkoani Pwani. 

Lori lililokuwa limebeba miili ya marehemu hao, likiwa linawasiri na kushusha maiti hao katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Taifa ya Muhimbili mchana wa leo. Jumla ya maiti 12 waliteremshwa kutoka katika gari hilo, huku ikisadikiwa kuwa maiti nyingine zaidi zingetarajiwa kufika hospitalini hapo. 

Maxmillian Kattikiro Blog (http://kattikirojrthedon.blogspot.com) tunawapa pole zetu za dhati wote ambao wanahusika na wamesikitishwa na msiba huu uliotokea, hususani wananchi na serikali ya Kenya kwa ujumla pia tunaungana nao na kuwaombea kwa mwenyezi Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu na awarehemu marehemu wote wa ajali hiyo mbaya ya kusikitisha. 

"Bwana Mungu alitoa na Bwana Mungu ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe" ........ Amina!

No comments:

Post a Comment