To Chat with me click here
Showing posts with label M4C. Show all posts
Showing posts with label M4C. Show all posts

Thursday, October 11, 2012

NYERERE AWAONDOA HOFU WAPIGA KURA


Mhe. Vicent Nyerere

MBUNGE wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (CHADEMA), amewaondoa hofu wananchi wa jimbo hilo, kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa na Chuo Kikuu cha Wauguzi iliyopo jimboni humo na kusema miradi hiyo ipo mbioni kuanza kutekelezwa.

Nyerere alisema hayo juzi alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara, uliofanyika kwenye viwanja vya Nyakato Shuleni mjini Musoma na kuongeza kuwa taratibu zote za kuanza ujenzi wa miradi hiyo imeshakamilika, kwani tayari wataalamu wa kusimamia ujenzi huo wameshafika mjini Musoma.

“Ujenzi wa hospitali yetu ya Rufaa ya Kwangwa na kile chuo cha Uuguzi ipo mbioni kuanza kujengwa. Taratibu zote za ujenzi zimeshakamilika na juzi juzi hapa wataalamu walifika kwa ajili ya upimaji tayari kwa utekelezaji wa kujengwa miradi hii ya maendeleo.“Lakini, natumia mkutano huu kuwaonya wana CCM wanaowapotosha wananchi kwamba eneo la hospitali na chuo hicho wamepewa wawekezaji. Huo ni uzushi na uongo mtupu. Siasa na uongo zisiwepo kwenye maendeleo, ni bora tutaniane sehemu nyingine, lakini isiwe kwenye maendeleo,” alisema.

Kwa upande mwingine, Nyerere aliwahakikishia wafanyakazi wa Kiwanda cha nguo cha Mutex kulipwa fidia zao, kwani alishazungumza na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, kuhusu kulipwa wafanyakazi hao na kwamba waziri huyo alihidi bungeni kwamba serikali itawaongezea fedha za fidia tofauti na ilivyowalipa awali.

Wednesday, October 10, 2012

M4C YAENDELEA VIJIJINI

Nyakatanga: Salehe Mashaka, Katibu wa Jimbo, Muleba Kaskazin
 Wana CCM 24 walirejesha kadi na kujiunga na CHADEMA

Monday, September 10, 2012

CHADEMA YAENDELEZA WIMBI LA KUIBOMOA CCM – UKONGA


Mhe. Kattikiro akiwa jukwaani akinadi sera za chama chake

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Ukonga jana kiliendeleza kile kilichokiita Mwendelezo wa uvunja na kuibomoa ng’ome ya CCM jimboni humo, katika harakati zake za kukiimarisha chama zaidi kwa operations zake za M4C.

Katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika viwanja vya mzambarauni, mgeni rasmi aitegemewa kuwa Mhe. Joshua Nassari (MB), lakini hakuweza kutokea kutokana na kuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Chama hapo jana. Hivyo basi wapambanaji wengine walishika nafasi hiyo ya kuendesha vuguvugu hilo la mabadiliko ambapo Diwani wa Viti maalumu, Mhe. Grace Shellukindo, Mhe. Maxmillian Kattikiro, Mwk. Wa Chadema Jimbo ndg. Michael Aweda, Katibu wa Jimbo ndg. Mwaipopo, Mwk. Wa Kamati ya Wahanga wa Mabomu G/mboto ndg. Obadia, aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la mvomelo ndg. Matokeo, Advocate Nixon, Mwk. Wa Bavicha Jimbo, ndg. Fredrick Kabati na wengine wengi walikuwepo ili kuweza kuisambaratisha vilivyo ngome hiyo ya CCM ambapo walifaulu kwa kiasi kikubwa sana. 

Akiongea katika mkutano huo Mhe. Kattikiro aliwataka CCM kuacha siasa chafu za kuchafuana zinazoendelezwa hivi sasa na watawala wetu na kusisitiza ni vyema watawala wakajikita zaidi katika kutafuta ufumbuzi juu ya kuwakwamua Watanzania toka katika wimbi kubwa la umasikini walilonalo. 

Aidha aliongeza kuwa, Tanzania ni nchi tajiri kuliko zote duniani, lakini utajiri wake umekuwa ukiwanufaisha watu wachache wenye madaraka na wageni ambao huingizwa nchini kwa kofia ya uwekezaji. 

Akitoa mifano kadhaa, alinukuu kauli ya Mheshimiwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuwa, “kama nchi yangu ingepewa bandari hii ya Dar-es-Salaam pekee, basi ningeweza kuifanya Rwanda moja ya mataifa tajiri mno duniani” hivyo alihoji je Tanzania tunabandari ngapi? Mtwara, Tanga, Zanzibar na Dar-es-Salaam, Je viongozi wetu hawana mawazo ya nini kifanyike kwa kutumia raslimali hiyo ya bandari kuweza kuinua uchumi wetu? Au vichwa vyao (Viongozi) vinautofauti gani na kichwa cha Kagame kuwa yeye awe na uwezo huo lakini watanzania tusiwe nao? Alihoji. 

Alisema, “Kauli ya Kagame, ilikuwa ikituambia watanzania kuwa, viongozi wenu mliowachagua (CCM) hawana nia ya dhati ya kuwakwamua toka kwenye umaskini uliowagubika watanzania, wako kwa ajili ya manufaa yao binafsi na ndiyo maana wameshindwa kutumia fursa mbalimbali za raslimali kemkem ambazo Tanzania imetunukiwa na Mwenyezi Mungu bure”.

Katika Mkutano huo wa hadara CHADEMA ilikuwa inawakaribisha wanachama wapatao 46 toka CCM na vyama vingine vya upinzani ambapo walisarimisha kadi zao kwa Mwenyekiti wa Jimbo Mhe. Aweda naye kuwakabidhi kadi ya chama hicho. 

Awada aliwapongeza sana makambanda hao wapya, ambao wameamua kishujaa kikihama chama tawala (Kuvua Gamba) na kuhamia chadema (Kuvaa Gwanda). 

Akizungumza kwa niaba ya wanaCCM ambao walijisalimisha kikamilifu kwa makamanda hao wa CHADEMA ambao walikuwa wakiendesha oparesheni hiyo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana wa CCM, alisema, 

“Tunawashukuru sana wanaCHADEMA kwa kutukaribisha CHADEMA, kwani CCM hakuna jipya ambalo sisi ambao tulikuwa wanachama wake tunaweza kulisema na kulisimamia. Kikubwa ambacho tumekiona huko (CCM) ni ufisadi na ubadhilifu wa mali za umma, wamekuwa wakijinufaisha wenyewe huku sisi wananchi tukibaki maskini siku hadi siku”. 

Hivyo aliwataka wanaCCM wengine ambao bado wanasitasita kukiunga mkono CHADEMA, wajitokeze na wasihofie mafisadi, kwani hawana nafasi tena katika nchi hii, kwani kwa miaka 50 ya utawala wao hakuna uwiano na maendeleo yaliyo fanyika kulinganisha na raslimali tulizonazo.
 
Habari katika Picha zaidi tafadhali bofya hapa.....

BINTI WA OSCAR KAMBONA AJIUNGA NA CHADEMA


Mwenyekiti wa Chadema UK, Chris Lukosi akimkabidhi kadi mwanachama mpya Neema Kambona, mtoto wa mwanasiasa mkongwe Mzee Oscar Kambona, shughuli fupi ilifanyika Barking baada ya watanzania wengi kuamua kujiunga na Chadema kupitia oparesheni zake za M4C zinaendelea.  

HECHE ALIZA WAKAZI WA KEKO ( TEMEKE)

MWKT WA BAVICHA TAIFA NDG JOHN HECHE jana amewaliza wakazi wa keko alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwa nia ya kupokea wanachama zaidi ya 51 walioamua kuvua gamba, kijana aliamua kusema misemo na falsafa nyingi zilizojikita kulaani wimbi la mauaji linalokuwa kwa kasi hapa nchini

1 "watu wabaya wanatamalaki siyo kwamba wana nguvu sana bali ni kwa sababu wema tumekaa kimya tukiwatazama"
 
2" polisi wameandaliwa kutuuwa mimi nasema watatuuwa sana lakini hawataua fikra zetu "
 
3"hatuko tayari tena kuona uhalifu huu ukiendelea mimi kama kiongozi wa vijana sasa niko tayari kuandamanisha mpaka watoto kudai haki ya kuishi ya watu inayotwaliwa na polisi" utekaji nyara , migomo, hali ya maisha kuporomoka na raisi kuwa omba omba nazo zilikuwa moja ya mazungumzo ya mh heche


Monday, August 27, 2012

POLISI WAZUIA MAANDAMANO YA CHADEMA


 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile.

WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kikitarajia kufanya mkutano mkubwa mjini Morogoro kuhitimisha operesheni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) iliyodumu kwa wiki tatu, Jeshi la Polisi mkoani hapa limejiingiza tena kwenye msuguano na chama hicho.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, amewakatalia CHADEMA kufanya maandamano wakati wakielekea kwenye uwanja wa mkutano wao leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege na kuwashirikisha viongozi wa juu wa chama hicho.

Agosti 4, mwaka huu, Kamanda Shilogile alizua tafrani wakati CHADEMA wakianza mikutano yao mkiani hapa, baada ya kuizuia akidai hawana askari wa kutosha kwani maonesho ya wakulima Nanenane yalikuwa yakiendelea.

MKUTANO WA CHADEMA, HOUSTON, TEXAS

Mh. Mbowe akimwaga sera za CHADEMA kwa wadau wa Houston 

 Sehemu ya umati wa wadau