To Chat with me click here

Tuesday, June 12, 2012

CHADEMA YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA BALOZI WA KENYA KUFUATIA KIFO CHA PROF. SAITOTI


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo kupitia Kurugenzi ya Mambo ya Nje ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imepokea kwa masikitiko ajali mbaya ya helikopta iliyokatisha uhai wa aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya, Profesa George Saitoti pamoja na Naibu wake, Orwa Ojode na maofisa wengine wa juu katika wizara hiyo. 

Kurugenzi ya Mambo ya Nje ya CHADEMA inatumia fursa hii kutuma salaam za rambirambi na pole kwa Balozi wa Kenya nchini na kuwatakia moyo wa subira wananchi wote wa Kenya katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mmoja wa wanasiasa na kiongozi wao mwandamizi.

Hayati Saitoti ambaye aliwahi kuwa makamu wa rais wa Kenya, alishikilia nafasi hiyo kwa muda wa miaka 13, pamoja na kuwa mmoja wa wanasiasa mwanamizi nchini Kenya, atakumbukwa pia kama mwanazuoni mahiri katika masuala ya uchumi, mahesabu na mtunga sera.

Imetolewa leo 12 juni 2012, Dar-es-Salaam na: 
Ezekieli Wenje (MB)
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA

No comments:

Post a Comment