Polisi wamdaka na watoto wake
SIKU
moja baada ya kundi la vijana wanaoaminika kuwa wanachama wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) kuwacharanga mapanga wafuasi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, sasa
ametishiwa kuuawa.
Habari
zinasema kuwa Diwani wa Kata ya Nduli, Idd Rashid Chonanga, jana asubuhi
alimvamia Mchungaji Msigwa ofisini kwake na kumtaka ajue kuwa siku zake
zinahesabika, hata kama juzi alinusurika, lakini atahakikisha ameuawa kwa njia
zozote zile, hali iliyomfanya mbunge huyo kukimbilia polisi kuomba msaada.
Diwani
huyo, ndiye anayetuhumiwa kusimamia kikamilifu tukio la kucharangwa mapanga kwa
wafuasi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati wa mkutano
wa mbunge huyo uliofanyika katika uwanja wa kata ya Nduli na kuwajeruhi vibaya.
Katika
mkutano huo ambao ulifanywa na mbunge huyo, mwenyekiti, katibu, wajumbe sita wa
CCM wa kata ya Nduli na wanachama wengine takriban 90 walihamia CHADEMA, huku
ikidaiwa kuwa wengine zaidi ya 150 wangelikihama chama tawala wiki hii.
Akizungumza
akiwa polisi, Mchungaji Msigwa alisema kuwa kauli ya diwani huyo imemtisha kwa
kuwa anajua ina baraka za viongozi wake wa ngazi ya juu.
Mchungaji
Msigwa alilitaka Jeshi la Polisi lisifanye mzaha katika jambo hilo, kwa kile
alichodai kuwa ni jambo la hatari na lenye lengo mahsusi la kuwatisha viongozi
wa vyama vya upinzani na wananchi baada ya kuona kuwa CCM inazidi kupoteza
maelfu ya wanachama wake kila kukicha.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, alisema hadi muda huo alikuwa
hajapokea taarifa hizo, lakini akaahidi kulishughulikia jambo hilo kikamilifu,
ili kulinda amani na usalama wa kiongozi huyo na raia wengine.
Hata
hivyo, Vyanzo vyetu vya habari vimethibitishiwa kukamatwa kwa diwani huyo na
vijana wa CCM waliohusika kuwakata mapanga watu watatu waliokuwa katika mkutano
wa mbunge huyo juzi.
Mmoja
wa maafisa wa polisi alidai kuwa miongoni mwa vijana waliokamatwa, wawili ni
watoto wa diwani huyo na kwamba watu wengine wanne, akiwemo mfanyakazi wa
diwani huyo, bado wanasakwa na jeshi hilo kwa kuhusina na tukio la juzi.
Akizungumzia
kutishwa kwa maisha kwa mbunge Msigwa, aliyekuwa mwenyekiti wa CCM kata ya
Nduli, Ayub Mwenda, alisema tangu jana amekuwa akipokea vitisho na kudai kuwa
hali hiyo haitakisadia chama tawala, badala yake kinasababisha kichukiwe na
hata na wale waliokuwa wakikipenda.
“Wananchi
wengi wamechukizwa sana na tukio la juzi, na wakisikia tena na hili alilofanya
huyu diwani leo, ndio itakuwa imezidi kujipalia mkaa. Hii ni nchi ya demokrasia
ya vyama vingi, na kila mtu anayo haki ya kujiunga na chama chochote, sasa
inashangaza kuona inakuwa nongwa kwao,” alisema Mwenda alipohojiwa na vyanzo
vyetu vya habari hili.
Wakati
huohuo, mmoja wa watu waliojeruhiwa vibaya katika shambulizi la mapanga juzi,
Osca Sanga bado amelazwa katika hospitali ya mkoa, wakati wengine wawili
waliruhusiwa jana.
No comments:
Post a Comment