Tawi la Chadema
Washington DC limepata Viongozi wapya walioshika nafasi za waliokuwa Viongozi
wa muda. Katika Uchaguzi huo Cosmas Wambura amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya
kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda Kalley Pandukizi.
Nafasi ya Katibu
imechukuliwa na Isidori Lyamuya aliyechukua nafasi ya Liberatus Mwang’ombe
aliyekuwa Katibu. Nafasi ya Mweka hazina imechukuliwa na Ludigo Mhagama na
nafasi ya katibu mwenezi imechukuliwa na Hussein Kauzella.
Nafasi nyingine
zilizogombewa ni Wenyeviti na Makatibu wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na
Wazee. Pia kulikuwa na nafasi ya Afisa Habari wa Chama. Akiongea baada ya
Uchaguzi Mwenyekiti aliyechaguliwa ndugu Cosmas Wambura amesema atatoa
ushirikiano mkubwa katika kuendeleza shughuli mbalimbaliza kukijenga Chama.
Pia
Katibu mpya amesema watashirikiana na Mwenyekiti na wanachama wengine wote
kuhakikisha Chama kinzidi kuwa Imara na kupata wanachama zaidi.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kalley Pandukizi (Kulia) akimkabidhi kitabu cha sera za Chama Mwenyekiti mpya Ndugu Cosmas Wambura.
Mwenyekiti Mpya wa Chadema Washington Cosmas Wambura akipeana mikono ya pongezi na Katibumpya Ndugu Isidori Lyamuya.
Kutoka kushoto Katibu mpya ndg. Isidori Lyamuya, Mwenyekiti mpya ndg. Cosmas Wambura, katibu wa zamani ndg. Liberatus Mwang'ombe na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake ndg. Kalley Pandukizi.
Baadhi ya wanachama walioshiriki katika zoezi la kupata uongozi mpya wa tawi hilo la Chadema Washington DC.
No comments:
Post a Comment