Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Bw. Nelson Mandela |
Rais
mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelezwa hospitali kwa siku ya pili
mjini Pretoria ambako alipelekwa Jumamosi.
Maafisa
wamesema kwamba amekuwa akifanyiwa uchunguzi, ingawaje haijajulikana kwamba ni
uchunguzi wa aina gani.
Rais
Jacob Zuma, aliyemtembelea Jumapili, alisema kwamba hali yake ilikuwa nzuri.
Bwana Mandela ana miaka 94.
Awali,
Mandela alilazwa hospitali mnamo Februari ili kutibiwa matatizo ya tumbo
yaliyokuwa yamemsumbua kwa muda mrefu.
Hajaonekana
hadharani tangu Afrika Kusini ilipofungua michezo ya Kombe la Dunia mwaka wa
2010.
No comments:
Post a Comment