|
Mr. & Mrs. Kattikiro Junior |
Tunapenda kuchukua nafasi hii, sisi kama familia kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo, wema, ulinzi, na baraka zake tele katika maisha yetu. Zaidi kabisa tunamshukuru kwa kutupatia zawadi ya "Baby Girl" - Maureen wakati huu.
Kwakweli, tungeweza kueleza mengi mno juu ya furaha kuu tuliyonayo kutokana na jambo hili kuu ambalo Mungu amelitenda katika maisha yetu. Tumekuwa na furaha hii kuu kwa sababu tunaamini kuwa ni baraka yake Mwenyezi katika maisha yetu. Lakini pia ni sababu ya magumu ambayo mama Maureen ameyapitia wakati wa ujauzito wake.
Lakini kwa neema na mapenzi ya Mungu, magumu na mashaka Mama Maureen aliyokuwa nayo, yalikoma siku ile ya tarehe 08 December 2012, majira ya 00:30hrs ambapo Maureen alikuja kwetu kama zawadi kwenye maisha yetu.
Tunapenda kuwashukuru wote waliokuwa wakitupa support wakati ule wa mapito magumu, hali kadhalika wakati wa kujifungua kwa Mama Maureen. Hatuna cha kuwalipa lakini tunawaombea sana kwa Mungu ili aendelee kuwabariki sana katika maisha yenu, awalipie kwa wema mlioutenda kwetu.
|
Maureen Kattikiro |
|
Maureen - akiwa amebebwa na bibi yake masaa machache baada ya kuzaliwa |
|
Maureen akiwa amelala huku akilindwa na bibi yake (Mama Nsanzugwanko) |
|
Baba na Mwana - kama waonekanavyo pichani |
|
Maureen akiwa amebebwa na dada yake Witness |
|
Beautiful Maureen sleeping! |
Woow congrats saaana!! Such an angel lovely.
ReplyDeleteLove yu twin. Kisses to preety maureen
Woow.
ReplyDeleteCongrats to the family. Proud of yu twin. Such a princess maureen. Kissesssss to lovey angel.
Linda
woow!! congrats to the family, proud of yu twin!! kissesss to preety lovely princess maureen
ReplyDeleteThanks so much @Linda, for such best wishes, Swthrt is taking care of Maureen, she will have your regards. Stay blessed.
Delete