Msemaji Msaidizi wa Jeshi la Polisi Nchini ASP Advera Senso |
Polisi
nchini Tanzania walikamata silaha haramu 439 kutoka kwa raia katika operesheni
ya mwezi mmoja ya kukusanya silaha zisizo vibali, alitangaza msemaji wa polisi
Advera Senso hapo Jumatatu.
Operesheni
hiyo ya polisi, iliyomalizika tarehe 5 Januari, iliwapa Watanzania fursa ya
kusalimisha silaha zao haramu bila ya kushitakiwa, liliripoti gazeti la The
Guardian la Tanzania. Miongoni mwa silaha zilizosilimishwa ni bunduki ndogo,
bunduki kubwa, bastola, risasi na maroketi.
Sasa
polisi wataanzisha msako wa nchi nzima na kuwakamata watu wanaoendelea kukaa na
silaha bila ya ruhusa maalum.
Polisi
iliwatolea wito raia kutoa taarifa juu ya yeyote mwenye silaha kinyume na
sheria. Mtanzania yeyote atakayetoa taarifa inayopelekea kukamatwa kwa mtu
atapewa zawadi ya kiasi cha shilingi 100,000 (dola 63), alisema Senso.
Kati
ya visa 876 za wizi wa silaha mwaka jana nchini Tanzania, 62 vilifanywa kwa
silaha haramu, kwa mujibu wa gazeti la The Guardian.
No comments:
Post a Comment