Moto mkubwa umewaka katika uwanja mkuu wa
ndege wa Jomo Kenyata mjini Nairobi Kenya , na kulazimisha kufungwa na hivyo
kusitishwa kwa safari za anga katika eneo la Afrika Mashariki.
Safari
za mamia ya wasafiri zimevurugwa na kuachwa nje ya uwanja huo wenye shughuli
nyingi zaidi Afrika mashariki . Nyingi kati ya safari za ndege zimeahirishwa
huku ndege zinazoingia zikielekezwa katika uwanja wa ndege wa Mombasa.
No comments:
Post a Comment