Aliyekuwa Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh |
Amesema
utendaji wa siku kwa siku wa mihimili hiyo unatakiwa kupimwa kwenye mizani ili
kila mhimili ufanye kazi bila kuingilia kazi za mihimili mingine kwani kwa
kufanya hivyo kutasaidia kulinda amani ya nchi pia kuongeza utawara bora na
wenye maadili mema.
Utouh
ameyasema haya leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kupokea tuzo ya
uadilifu na utawala bora kutoka kwenye kampuni ya Dream Success
Enterprises baada kuutambua umuhimu wa utendaji kazi wake akiwa kazini kabla ya
kustaafu.
Amesema
ubabe na kutoelewana huku kila mhimili ukitaka kujiona kuwa upo juu ya muhimili
mwingine kuna weza kukaleta machafuko makubwa yatakayoigharimu nchi, na kwamba
kurudisha amani itachukua muda.
“Kuna
haja ya hiii mihimili kufungiwa mizani, kufanya kazi kwa kutoingiliana, pia
ikiheshimiana na kutatua mambo yao kwa hekima Tanzania itakuwa sehemu tulivu,
yenye amani na kimbilio la wanyonge, lakini kama kila muhimili ukifanya kazi
kivyake bila kuzingatia sheria machafuko yanaweza kutokea na kuifanya nchi
isitawalike,”anasema Utouh.
Anasema
katika harakati zake akiwa kazini atalikumbuka daima sakata la uchotwaji wa
fedha katika akaunti ya nje (EPA) pamoja na ripoti ya aliyekuwa katibu Mkuu wa
Nishati na Madini David Jairo.
Anasema
hayo yote yaliwezekana kufanyika kwa sababu mihimili ya Serikali ilikuwa
ikifanya kazi zake kwa weledi wa hali ya juu bila kuingiliana katika maamuzi.
Anasema
tuzo aliyopata anaipokea ingawa katika kipindi chake cha kazi ndipo
kulipozaliwa jina la ufisadi, hata hivyo amesema anajivunia kuwepo kwake katika
ofisi ya CAG kwani alifanikwia kurudisha imani ya chombo hicho kwa wananchi na
hivi sasa wananchi wanakiamini.
No comments:
Post a Comment