To Chat with me click here
Showing posts with label Chadema. Show all posts
Showing posts with label Chadema. Show all posts

Friday, July 26, 2013

CHADEMA YAIKOROGA POLISI!



UAMUZI wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukataa kuwasilisha ushahidi wa mauji ya mlipuko wa bomu uliotokea jijini Arusha, umeliweka njia panda Jeshi la Polisi na hivyo kushindwa kuchukua hatua.

Licha ya jeshi hilo kumhoji Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na kumtaka awasilishe ushahidi huo, kiongozi huyo amekataa agizo hilo akisema kuwa wamekubaliana kuutoa ushahidi huo kwa tume huru ya majaji endapo Rais Jakaya Kikwete ataiunda kama walivyomuomba.

Chanzo chetu ndani ya jeshi hilo, kimedokeza kuwa msimamo huo wa CHADEMA umeliweka njia panda na hivyo kushindwa kuchukua hatua za kuwabaini watuhumiwa wa tukio hilo na kuwafungulia mashtaka kutokana na mkanganyiko wa taarifa zinazotolewa.

Jeshi hilo linadaiwa kuwa awali lilitaka kujiegemeza kwenye kauli za kisiasa za baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali ili kuonyesha kuwa CHADEMA ilisababisha mlipuko huo yenyewe kwa ajili ya kuwahadaa wafuasi na kujitafutia umaarufu.

Hata hivyo, mbinu hiyo ya kutaka kuwasakama baadhi ya viongozi na wafuasi wa CHADEMA inadaiwa kufifishwa na tamko la Mbowe pamoja na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kwamba chama kina ushahidi unaoonyesha kuwa tukio hilo lilifanywa na polisi.

“Hapa kuna mkanganyiko hasa baada ya Mbowe kudai wanao ushahidi wa video ya tukio hilo. Wakubwa wetu wamegawanyika na kujikuta wakitoa kauli za kukinzana maana wanahofia wakiwafungulia kesi watu wengine mashtaka halafu CHADEMA ikaonyesha ushahidi tofauti itakuwa ni aibu,” kilisema chanzo chetu.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, jeshi hilo mkoani Arusha lilikuwa limewakamata watu wawili raia wa kigeni likiwatuhumu kuhusika na mlipuko huo lakini baada ya Mbowe kugoma kupeleka ushahidi huo, watuhumiwa hao hawakuweza kufunguliwa mashtaka.

Pia katika hali ya kushangaza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa makachero wa Taasisi ya Uchunguzi ya Marekani (FBI) wamefika mkoani Arusha kuchunguza jambo hilo.

Hata hivyo taarifa kutoka ubalozi wa Marekani zilikana FBI kuingia nchini kuchunguza jambo hilo hivyo kusababisha mkanganyiko wa tukio hilo lililovuta hisia kubwa ndani na nje ya nchi.

CHADEMA mara kwa mara imekuwa ikilituhumu jeshi la polisi na makada wa CCM kuendesha harakati za kukidhoofisha kwa kutumia matukio mbalimbali yanayofanywa na chama hicho cha upinzani.

Mmoja wa viongozi wa CHADEMA aliviambia vyanzo vyetu vya habari, kuwa polisi walikuwa wamepanga kuwatumia FBI kuuhabarisha umma kuwa CHADEMA ilihusika na ulipuaji huo bomu lakini kutokana na mazingira yaliyopo wameshindwa kutekeleza uovu huo.

“Unajua hila za polisi na CCM kila siku zinabadilika lakini kwa bahati mbaya hawajui kuwa wananchi wanajua kinachofanyika, kuna askari hawaridhiki na uovu unaofanywa na wenzao,” alisema kiongozi huyo.

Thursday, June 13, 2013

TAARIFA KWA UMMA!


KUHUSU KAMANDA LWAKATARE; PRESS CONFERENSE NA MIKUTANO YA KAMPENI
Kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari tangu jana juu ya vitu viwili ambavyo vyote vinamhusu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Ndugu Wilfred Mganyizi Lwakatare.

1. Kwamba atafanya press conference leo, (watu wale wa upande wa pili wameenda mbali hata wametaja muda eti ni saa 4 asubuhi)

2. Atakuwa kwenye mizunguko ya mikutano ya kampeni katika chaguzi ndogo za udiwani zinazoendelea katika hatua ya lala salama maeneo mbalimbali nchini.

Usahihi.

Kwa kuzingatia masuala kadhaa hasa mikakati ya kitaalam katika mapambano ya kisiasa, hususan katika suala hili, press conferense iliahirishwa tangu jana mapema asubuhi, baada tu ya baadhi ya vyombo vya habari kuwa vimetangaza kuwa itafanyika leo, Alhamis. Tuliviarifu vyombo vya habari hivyo. Imesogezwa mbele na taarifa zitatolewa tena.

Suala la mizunguko kwenye kampeni za uchaguzi mdogo...hakuna kitu kama hicho kwa sasa.

Pamoja na kwamba kuna watu wenye mapenzi mema kabisa na vuguvugu la mabadiliko wamekuwa na hamu ya kutaka kumsikia kamanda mwenzao, ndugu Lwakatare akizungumza majukwaani baada ya miezi mitatu ya 'ukatili' mkubwa, pia tumebaini kuwa watu wa upande wa pili, wanataka sana kujua CHADEMA sasa inajua kiasi gani juu ya njama za kuibambikia ugaidi, utekaji na mauaji.

Hivyo upande huo wa pili, ambao unaonekana dhahiri kuwa under pressure ya kutojua kiasi gani mipango yao inajulikana na itaumbuliwa kwa kiwango kipi, umekuwa ukieneza habari za Lwakatare kufanya mikutano ya hadhara kwenye kampeni za uchaguzi wa madiwani, kitu ambacho si kweli.

Baada ya hila na uovu wa watawala na vibaraka wao kushindwa katika jaribio lingine kubwa kabisa wao kuwahi kupanga dhidi ya wimbi la mabadiliko na kutaka kuzuia kasi ya CHADEMA kuwaondoa madarakani, tumwache ndugu Lwakatare apumzike na familia, wakati mipango makini ikifanywa kwa ajili ya matukio yote mawili ambayo Watanzania wanategemea na kuyasubiri kwa hamu yafanyike; mkutano na press conference.

Kitu kimoja cha uhakika ni kwamba, watu wa upande wa pili, ambao tayari hofu yao inajulikana, hawataweza kumchagulia Lwakatare wala kuichagulia CHADEMA kitu gani cha kusema, kama ambavyo wameanza kufanya kupitia forums mbalimbali. Let tthem cool down, wasiwasi wa nini! Yote yakayosemwa itakuwa ni kwa ajili ya maslahi ya Watanzania, haitakuwa kwa ajili ya kuifurahisha 'status quo'.

Ukweli haujawahi kushindwa na uongo, wala dhuluma haijawahi kuishinda haki. Vyote viwili, ukweli na haki, vinaweza kuchelewa tu, lakini hatimaye huwadia. Kwa sababu Lila na Fila havitangamani.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari - CHADEMA
Alhamis, Juni 13, 2013.

Friday, May 31, 2013

CHADEMA YAAHIDI KUJENGA ZAHANATI TINGENI



MRATIBU wa kampeni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Tanga, Jonathan Bahweje, ametoa ahadi ya kujenga zahanati ya kata ya Tingeni katika jimbo la Muheza.

Bahweje alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani kata ya Tingeni, Omary Kanyau, uliofanyika kijiji cha Ukoka.

Alisema wananchi wa kata hiyo wanauhitaji mkubwa wa huduma za afya kwani zilizopo ziko mbali na kwamba chama hicho kina mipango endelevu na wananchi hao.

Akizungamza kwa niaba ya wakazi wanaoishi katika kata hiyo, Shaban Salim, alisema kwa muda mrefu wanateseka bila kupata huduma za afya, hivyo kuwalazimu kwenda kutibiwa katika hospitali teule ilioko wilayani Muheza.

Salim alisema katika kata hiyo mbali na huduma za afya kuna tatizo la daraja ambapo likijaa maji huwezi kuvuka kwenda upande wa pili kitendo kinachopelekea watoto wanaosoma shule katika maeneo hayo kushidwa kuhudhuria masomo kutokana na daraja hilo kujaa maji.

Wednesday, May 22, 2013

PROFESA J AAMUA KUJIUNGA NA CHADEMA RASMI!


Profesa J akipokea Kadi ya CHADEMA toka kwa Mhe. Mbilinyi a.k.a SUGU

MSANII maarufu wa hip hop nchini, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay, au Jay wa Mitulinga, pamoja na msanii wa kundi la Mapacha, Levison Kasulwa wamekabidhiwa rasmi kadi za kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mjini Dodoma jana.

Zoezi hilo lilifanyika katika hoteli ya Desert Palm, ambako walikabidhiwa kadi hizo na Mbunge wa Mbeya Mjini, ambaye pia ni Waziri Kivuli, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Akizungumza baada ya kukabidhi kadi hizo, Sugu alisema wasanii hao wameamua uamuzi wa busara, kwani CHADEMA ni chama cha kutetea haki za wanyonge na wasanii kwa ujumla.

Sugu alisema yeye alipofikia uamuzi wa kujiunga na CHADEMA, alipokelewa na kupewa ushirikiano mkubwa na makamanda wote ambao sio wasanii, hali inayoonesha kuwa chama hicho hakina ubaguzi kwa mtu yeyote.

“Naamini kamanda licha ya kujiunga huku, lakini utaendeleza muziki na utashirikiana kwa hali na mali kupeleka mbele gurudumu la chama na Watanzania kwa ujumla,” alisema Sugu.

Waziri kivuli huyo aliongeza kuwa kama angeambiwa amshauri Profesa Jay, angemwambia arudi nyumbani Mikumi akawatumikie wananchi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, akizungumza katika hafla hiyo, alisema yeye ni mmoja kati ya watu waliowashawishi wasanii hao wawili, Profesa Jay na Sugu kujiunga na CHADEMA.

Alisema baada ya kuwashawishi, Mbilinyi ilimchukua miaka mitano kufikia uamuzi wa kuwa mwanachama, wakati Profesa Jay imemchukua miaka sita hadi jana alipoamua kufikia uamuzi huo, kitendo ambacho kinaonesha dhahiri kuwa kuchukua kwao muda mrefu ni kwa dhati na wala hakutetereki.

“Mtu yeyote anayefanya uamuzi kwa muda mrefu, anakuwa amefanya uamuzi sahihi na wa uhakika na anakuwa anajiamini katika uamuzi huo,” alisema Mnyika.

Naye Profesa Jay, alisema atailinda kwa gharama yoyote CHADEMA na atakuwa tayari kushirikiana na wapiganaji wenzake ambao ni makamanda ndani ya chama hicho, katika kuhakikisha inasonga mbele na kuendelea kutetea haki za Watanzania.

“Mimi Profesa Jay ni kama daraja, nawahamisha watu wa upande huu na kuwapeleka upande mwingine wa sarafu,” alisema.
Kaselwa wa Mapacha, alisema ameamua kwa moyo wake mwenyewe na wala hajashinikizwa na yeyote kujiunga na chama hicho.

ILI TUENDELEE TUNAHITAJI VITU VINNE, KWANZA WATU, PILI ARDHI, TATU SIASA SAFI, NNE UONGOZI BORA - PROF J

Friday, May 17, 2013

WAGOMBEA UDIWANI WA CHADEMA - KANDA YA KASKAZINI




TAARIFA KWA UMMA
 WAGOMBEA WA UDIWANI - KANDA YA KASKAZINI

Tarehe 15 Mei 2013, wagombea wafuatao wa CHADEMA walipitishwa na TUME YA UCHAGUZI kuwania nafasi za uwakilishi (UDIWANI) katika maeneo ya kata mbalimbali za kanda ya Kaskazini. Wagombea hawa walipita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Chama kina matarajio makubwa sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi watapata fursa nzuri ya kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana dhamira njema sana na ya kweli katika kuwatumikia.

Wagombea waliopitishwa pamoja na mikoa yao ni:

JINA LA MGOMBEA
KATA
JIMBO
MKOA
BI. YOSEPHA KOMBA
GENGE
MUHEZA
TANGA
BW. OMARI HATIBU SALIMU
TINGENI
MUHEZA
TANGA
BW. LAWRENCE SURUMBU TARA
BASHNET
BABATI VIJIJINI
MANYARA
BW. ERNEST JOROJIK
DONGOBESH
MBULU
MANYARA
ENG. JEREMIAH MPINGA
ELERAI
ARUSHA MJINI
ARUSHA
BW. RAYSON NGOWI
KIMANDOLU
ARUSHA MJINI
ARUSHA
BW. MALANCE KINABO
THEMI
ARUSHA MJINI
ARUSHA
BW. EMMANUEL KESSY
KALOLENI
ARUSHA MJINI
ARUSHA
BW. JAPHET SIRONGA LAIRUMBE
MAKUYUNI
MONDULI
ARUSHA

CHAMA kimejipanga kushiriki uchaguzi huu kikamilifu sana na katika maeneo yote kanda imeteua MAMENEJA WA KAMPENI ili kuhakikisha uratibu na utekelezaji wa kampeni kwa mfumo tuliouweka.

Imetolewa leo tarehe 16 Mei 2013.
Amani Golugwa
Katibu wa Kanda ya Kaskazini