Zanzibar
imepanga kuzindua miradi 62 ya maendeleo wakati wa wiki ya kuelekea siku ya
uhuru tarehe 12 Januari, kwa kuanza na zoezi la kufanya usafi nchi nzima
(tarehe 4 Januari).
Siku
ya Jumamosi, Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein atafungua jengo jipya la
Taasisi ya Utawala wa Umma huko Tungu, na kituo kipya cha udhibiti wa serikali
huko Mazini, yote yalijengwa kwa fedha kutoka serikali ya China.
Makamu
wa Rais wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal atafungua hoteli ya kitalii ya nyota
tano katika kijiji cha Nungwi siku ya Jumapili, na siku inayofuata ya Alhamisi
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete atafungua shule mpya inayoitwa Mlimani.
Viongozi
mashuhuri wa serikali wa Zanzibar na Tanzania wataendelea kuongoza katika
uzinduzi wa miradi kama hiyo kwa wiki nzima, ikiwa ni pamoja na shule za
sekondari, maabara za uchunguzi na mabweni ya wanafunzi.
Waziri
wa Nchi anayeshughulikia Matukio ya Kitaifa Mohamed Aboud Mohamed alitetea
sherehe hizo za muda mrefu, ambazo zinakadiriwa kugharimu shilingi milioni 600
(dola 380,000). "Tusifikirie kwamba fedha zinatumiwa kupita kiasi,
zinatumiwa katika miradi ya maendeleo," alisema.
No comments:
Post a Comment