Mwili wa Zenawi ukiwasili Adis Ababa
Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa
Ethiopia, Melez Zenawi, uliwasili jana usiku katika mji mkuu wa nchi hiyo Adis
Ababa na kwa sasa umehifadhiwa katika Ikulu hadi mazishi yake yatakapofanyika.
Maelfu
ya raia wa nchi hiyo walimiminika katika barabara za mji huo jana jioni wakati
mwili wake ulipowasili kutoka mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.
Meles,
ambaye alikuwa na umri wa miaka 57, aliaga dunia ghafla kutokana na maambukizi
wakati alipokuwa akitibiwa.
Kifo
cha Bwana Zenawi kimezua hofu ya kugombea madaraka hali ambayo ingeweza
kuathiri amani ya nchi hiyo.
Kwa
mujibu wa vyombo vya habari, naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn ataliongoza
taifa hilo hadi mwaka 2015 wakati uchaguzi mkuu utakapofanyika.
Utawala
wa Bwana Zenawi ulishutumiwa kwa kukandamiza upinzani na kuna hofu kuwa Waziri
Mkuu mpya huenda asiwe na uzoevu wa kushughulikia na kutatua uhasama wa kisiasa
unaoendelea nchini humo.
Zenawi
amesifika kwa kuiongoza Ethiopia kufikia mafanikio makubwa ya maendeleo na
uchumi, lakini wakosoaji wake wanasema licha ya hayo yote utawala wake
haukuruhusu uhuru wa siasa za vyama vingi na kuwa viwango vya ukiukwaji wa haki
za binadam bado viko juu.
Bwana
Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo lilipoingia vitani na
nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.
Meles
Zenawi aliingia madarakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi lakini akapokea sifa
kutoka kwa mataifa ya magharibi.
No comments:
Post a Comment