Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mpango wa kugawa
ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha
(Longido,Monduli na Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha
mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.Kulia
kwake ni Mbunge wa Jimbo hilo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Kushoto
kwake ni WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge),
William Lukuvi.
Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Waziri Mkuu mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa baada ya kufanyika kwa
mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za
Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000
kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Baadhi ya
Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Arusha waliofika katika kijiji cha
Makuyuni,Wilayani Monduli kumlaki.Rais Kikwete leo amefika katika kijiji
hicho cha Makuyuni na kuzindua mpango wa kugawa ng’ombe 1500 kila mwezi
kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha (Longido,Monduli na
Ngorongoro) kama kifuta jasho cha kupoteza mifugo 800,000 kutokana na
ukame na athari zake zilizotokea mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha
Makuyuni,Wilayani Monduli leo wakati alipofika kuzindua mpango wa kugawa
ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha
kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na
ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Rais Kikwete akiwa na Viongozi wengine Meza kuu.
Rais Kikwete akielekea kwenye Jukwaa lililoandaliwa kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Monduli
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Makuyuni Wilayani Monduli leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akitoa shukrani kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete kwa kuweza
kuwakumbuka wananchi wa Wilaya ya Mbonduli.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa akipatiwa maelezo ya Mifugo hiyo kabla Rais Kikwete hafafika na
kuigawa kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho
cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake
uliozikumba wilaya hizo mwaka 2008/2009.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigawa Ng’ombe kwa wananchi wa
wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha
mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Wananchi wa Kijiji cha Makuyuni wakifatilia zoezi la ugawaji wa Ng’ombe.
Rais Kikwete na mtoto
Wakinamama wa jamii ya kimasai wakiimba nyimbo za kumkaribisha Mh. Rais.
Burudani kutoka kwa Vijana wa JKT.
No comments:
Post a Comment