Wafuasi wa CDM wakiwa kwenye maandamano kuelekea viwanja vya mkutano kabla ya vurugu kutokea |
Dr. Slaa akihutubia maelfu ya wanachama na wananchi wengine katika mkutano huo baada ya fujo za awali za mabomu ya polisi. |
Niliwahi
kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali imeanza
kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza kuongoza serikali
kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama chama cha mauaji.
Raia
watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya yamefanyika
kwenye maandamano ya amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa CHADEMA kuelekea
kwenye mkutano.
Vurugu
zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video. Vyanzo
vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za kuwasha toka Dar
Es Salaam.
Tuombe
MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara ambao wananchi wamekusanyika kwa
wingi hivi sasa. States captured by grand corruption of the ruling party
cronies for so many years’ resorts to bullets as a way of stopping M4C through
the ballot.
Maisha ya
wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.
John John MNYIKA,
27 Agosti, 2012
No comments:
Post a Comment