Mabaki ya Helikopta mbili za Uganda
ambazo ziliripotiwa kutoweka siku ya Jumapili zimepatikana mashambani nchini
kenya.
Kanali
Cyrus Oguna ambae ni msemaji wa jeshi la Kenya amesema hatma ya watu 14
waliokuwemo ndani ya chombo hicho haijulikani. Ndege
hizo mbili zilikuwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikipelekwa nchini Somalia
kuongezea nguvu kikosi cha umoja wa Afrika kilichoko huko.
Helikopta
ya tatu ambayo pia ilikuwa katika msafari huo ilitua kwa ghafla katika eneo la
mlima Kenya siku ya Jumapili. Kanali
Oguna amesema wote waliokuwa katika helikopta hiyo ya tatu waliokolewa.
Ni
helikopta moja peke yake ndio faulu kutua vizuri na kuongeza mafuta katika mji
wa Garissa ulioiko kaskazini mwa Kenya. Helikopta
hizo nne ambazo zimetengezezwa Urusi ziliondoka siku ya Jumapili Uganda
zikelekea Somalia kabla ya kukumbwa na mkasa huo.
Masalia
ya helikopta hizo mbili ambazo awali ziliripotiwa kutoweka zilionekana juu ya
mlima Kenya na maafisa wa Shirika la Wanyama pori, limeripoti gazeti la Daily
Nation la Kenya. Msemaji
wa jeshi Kanali Oguna ameimbia BBC kwamba kikosi cha jeshi la Kenya linaelekea
katika eneo hilo la Mlima Kenya , ambao ndio mlima wapili kwa urefu, Afrika.
Afisa
huyo amefafanua kwamba moja ya helikopta hizo imeharibika kabisa ilhali ya pili
imeharibika kiasi. Helikpta
hizo zilikuwa zinaelekea nchini Somalia kuongezea nguvu vikosi vya Umoja wa
Afrika ambavyo vinajitayarisha kuvamia mji wa Kismayo na kuwafurusha wapiganaji
wa Al Shabaab toka mji huo ambyo ndio ngome yao kuu.
No comments:
Post a Comment