Israili imekasirishwa na uwamuzi wa
serikali ya Afrika ya Kusini wa kupiga marufuku nembo zinazowekwa kwenye bidhaa
ambazo zina nembo isemayo ''made in Israel'' il hali zimetengenezwa Ufuko wa
magharibi. Badala
yake Afrika ya Kusini inataka bidhaa hizo zibainishwe kwa kuandikwa kuwa
zimetengezwa katika ''maeneo yanayokaliwa''
Wizara
ya mashauri ya nje ya Israil itaja hatua hiyo kama ya ubaguzi. Makaazi,
miji ya Israili iliyojengwa katika maeneo yanayozozaniwa ya wa Palestina ni
kinyume cha sheria ya Kimataifa ingawa Israili inapinga hilo. Afrika
ya Kusini inaaminika kuwa nchi ya kwanza kujaribu kutimiza uamuzi huu kisheria
ingawa serikali nyingine kama Uingereza, zimewahi kuyashauri maduka makubwa
yabainishe bidhaa zitokazo kwenye makaazi ya walowezi wa Israili. Lakini
kuanzia leo nchini Afrika ya Kusini, bidhaa kutoka makaazi hayo ya Israili,
hazitokubalika kuwa na nembo "made in Israel".
Wizara
ya mashauri ya nje ya Israili, imeutaja uwamuzi huo kama wa Ubaguzi wa rangi na
usiokubalika. Wizara
hiyo imemtaka Balozi wa Afrika ya kusini nchini Israili aeleze hatua ya
serikali yake. Kuna
kampeni inayofanywa miongoni mwa wa Palestina na waungaji mkono wao ya kususia
bidhaa zinazotengenezwa ndani ya maeneo yanayokaliwa na walowezi wa Kiyahudi
pamoja na Israili kwa ujumla.
Msemaji
wa vuguvugu la Afrika ya Kusini ameutaja uamuzi wa Afrika ya Kusini kama ishara
tu lakini akaonyesha matumaini utakua chachu kwa wengine.
Raia
wa Palestina wanaopendelea vikwazo mara kwa mara hutumia mfano wa juhudi za
uhuru huko Afrika ya Kusini kama changamoto na kuishutumu Israili kuwa
inaendesha sera ya ubaguzi na kuongoza dola la kiimla, Israili inapinga tuhuma
hizo.
No comments:
Post a Comment