Pichani
ni kijana aliyeelezwa kupigwa risasi kichwani katika tafrani hizo na baadae
kupoteza maisha Ametambulishwa kwa jina la Ally Zona, ambae alikuwa anauza
magazeti katika stendi ya Msamvu. Tukio hili lilitokea mapema jana asubuhi
kuelekea saa sita mchana wakati Polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi hao wa
chadema. Mtoa taarifa anasema Polisi wanadaiwa kutumia risasi za moto pamoja na
mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamani hao.
Watu wengine waliojeruhiwa katika tafrani hiyo wameelezwa kuwa ni mwendesha baiskeli Hashim Seif ambae amejeruhiwa kwa risasi mguuni akiwa napita na baiskeli yake na kijana mwingine aliielezwa kuwa ni muuza matunda Frank Valimba ambae amejeruhiwa na risasi tumboni.

inaendelea fuata link hii
Mmoja
wa wadau wa Maxmillian Kattikiro Blog alipohojiwa na mwandishi wetu alikuwa na
haya ya kusema:
“Polisi wanachafua mji sasa, polisi
wanawapitisha wana-Morogoro kwenye tanuru ambalo watu wa Mwanza, Mbeya, Arusha,
Moshi, Musoma, Tarime, Ruaha na kwingineko kwingi, walipita/kupitishwa ili kuwa
hapo walipo wakiwa na imani isiyoyumba katika mapambano haya ya kudai na
kuwaandaa Watanzania kwa mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala. Chuma
hakiwezi kuwa chuma mpaka kipite kwenye tanuru, lakini why doing it
unnecessary?”
TAMKO KUTOKA TANZANIA
JOURNALIST ALLIANCE (TAJOA)
Jumuia ya Waandishi wa Habari Tanzania (Tajoa) inalaani kwa nguvu zote mauaji
ya makusudi yaliyofanywa na Jeshi la Polisi leo mjini Morogro. Inashangaza
Tanzania sasa inataka kugeuka taifa la polisi wauaji. NI vyema busara, ujuzi na
mbinu stahiki zikatumika badala ya kuendelea kuua raia hata wasiokuwa na hatia.
Hebu ona huyu masikini alivyouawa kwa kupigwa risasi kwenye paji lake la uso na kumsab
Hebu ona huyu masikini alivyouawa kwa kupigwa risasi kwenye paji lake la uso na kumsab
abishia
kifo cha papo hapo. Inaelezwa alikuwa muuza magazeti aliyekuwa kibandani kwake.
Sasa tusubiri taaria ya Polisi ambayo huenda ikasema alikuwa amebeba silaha.
Tanzania, tusikubali kuwa taifa la polisi wauaji.
Marafiki wa Tajoa, nini sasa kifanyike kukomesha hali hii ambayo inaonekana kuota mizizi? Toa maoni yako hapa ili nasi tuyapeleke kwa Jeshi la Polisi
Tanzania, tusikubali kuwa taifa la polisi wauaji.
Marafiki wa Tajoa, nini sasa kifanyike kukomesha hali hii ambayo inaonekana kuota mizizi? Toa maoni yako hapa ili nasi tuyapeleke kwa Jeshi la Polisi
Wafuasi wa CHADEMA wakiwa katika maandamano hayo mjini Morogoro. |
Moshi wa mabomu uliolipuka kutawanya maandamano ya CHADEMA jana Morogoro |
Akina mama na watoto wakijaribu kukimbia mabomu ya machozi hapo jana. |
No comments:
Post a Comment