CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakikuridhishwa na hukumu iliyotolewa na
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga, Peter Dalally
Kafumu.Taarifa iliyolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye mchana leo, imeseme kufuatia kutoridhishwa na hukumu
iliyotolewa jana na Jaji wa Mahakama hiyo, Mary Shangali, kitakata
rufani.
“Chama
Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana Agosti
21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora. Kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa
kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Mbunge wa jimbo la
Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter Kafumu.Kusudio hilo linatokana na
kutorishwa na hukumu hiyo”. imesema taarifa hiyo.
Jana
Jaji Mary Shangali katika hukumu yake, alisema ametengua ushindi wa Dk.
Kafumu baada ya kurishishwa na madai saba kati ya 17 yaliyowasilishwa katika
mahakama hiyo na Mlalamilikaji, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Chadema, Joseph
Kashindye.
Dk.
Kafumu wa CCM alitangazwa kushinda kiti na Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la
Igunga, katika uchaguzi mdogo uliofanyika, Septemba mwaka jana, baada ya
kujiuzulu aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Rostam Aziz.
No comments:
Post a Comment