Rais Mohammed Morsi wa Kushoto akibadilishana mawazo na baadhi ya maofisa wake. |
Rais wa Misri, Mohammed Morsi,
ameikashifu serikali ya Syria na kusema kuwa inatumia mabavu.
Rais
Morsi aliyasema hayo katika hotuba yake nchini Iran ambayo ni mshirika mkubwa
wa Syria.
Morsi
alisema kuwa ni wajibu wa kila mtu kuunga mkono upinzani nchini Syria ili
uungane dhidi ya kile alichokitaja kama utawala wa kimabavu.
Katika
hotuba yake katika mkutano maalum mjini Tehran, bwana Morsi alisema kuwa ni
jukumu lao kimaadili kuunga mkono upinzani nchini Syria sawa na kuwa mkakati
sawa wa kisiasa.
Waziri
wa mambo ya nje wa Syria, Walid Mouallem, alisema kuwa wajumbe wa Syria
waliondoka kwenye mkutano huo wakati wa hotuba ya rais Morsi, ambayo aliitaja
kama ya uchochezi wa kuendelea kumwaga damu ya wananchi wa Syria.
Ziara
ya rais Morsi ni ya kwanza ya afisa mkuu wa Misri, tangu mapinduzi ya kiisilamu
mwaka 1979.
Chanzo: BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment