Dk. Steven Ulimboka amerejea leo nchini
na kutoa shukrani za dhati kwa watanzania kwa dua na michango yao kuinusuru
afya yake na kuahidi kuendeleza mapambano dhidi ya huduma bora za afya na
maslahi kwa madaktari.
Ulimboka amerejea nchini wakati jamii
bado ikiwa katika kizungu mkuti cha nani hasa aliyemteka na kumpa mateso makali
Dk. Steven Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini na kiu
ya wananchi sasa ni kutaka kujua ukweli kupitia kwake.
Daktari huyo ambaye amejizolea umaarufu
nchini kwa harakati za kudai haki na maslahi ya madkatari na huduma bora
Hospitalini amerejea Jana jijini Dar es Salaam akitokea nchini Afrika kusini
ambako alipelekwa na Madaktari wenzake tangu Juni 30 mwaka ambako alikuwa
akitibiwa majeraha aliyoyapata baada ya kutekwa na kundi la watu wasiojulikana.
Dk. Ulimboka alitekwa, kupigwa na
kutelekezwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaa lilidai kuwa aliyemteka daktari
huyo ni raia wa Kenya ambaye tayari wanamshikilia.
Dk. Ulimboka amewasili Jana majira ya
saa 8 alasiri katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es Salaam na SA Airways na kulakiwa kwa shangwe, hoihoi nderemo na
vifijo kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki sambamba na madaktari wenzake na
wanaharakati.
Hakika Mungu yupo! Na anatenda miujiza
yake, Ulimboka inakumbukwa aliondoka nchini akiwa hajiwezi kutokana na hali
yake kuwa mbaya na kubebwa katika machela lakini leo amerejea mzima wa afya na
anatembea mwenyewe.
Licha ya vurugu za hapa na pale ambazo
zilikuwa zikisababishwa na ndugu na jamaa ambao walitaka wanahabari wasilidake
tukio hilo la kihistoria mithili ya Mtanzania kutwaa medali ya Dhahabu Olympic
2012 huko London lakini paparazi waliweza kunasa taswira kadhaa na kuongea nae.
“Nimepona ndugu zangu….nawashukuru
nyote mlioniombea, watanzania, madaktari, ndugu na jamaa zangu nashukuru pia
kunisaidia kupata matibabu bora hadi leo hii narudi nyumbani, niko fiti
nikitembea mwenyewe,” alisema Dk. Ulimboka.
Miongoni mwa wana harakati ambao Maxmillian
Kattikiro Blog ilifanikiwa kuwaona uwanjani hapo ni pamoja na Mkurugenzi wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Usu Malya na Mkurugenzi wa Chama cha
Waandishi wa Habari wanawake (TAMWA).
Ananileya Nkya, ambaye yeye alisema kuwa
sasa ndiyo mapambano na harakati za kweli za ukombozi na utetezi wa haki za
Watanzania ndiyo unaanza. Aliongeza kuwa, walidhani wangeweza kumaliza matatizo
yanayoliandama Taifa kwa kutumia nguvu za kimamlaka walizonazo, lakini kurudi
kwa Dr. Ulimboka mzima tena akiwa anatembea yeye mwenyewe kunaonesha jinsi gani
walivyoshindwa. Hivyo vita hiyo ndo inaanza upya tena kwa nguvu zaidi.
Wanaharakati hao walijipamba na mabango
kadhaa yaliyo kuwa na jumbe za “Dk Ulimboka karibu nyumbani uliumizwa kikatili
ukitetea afya bora kwa watanzania.” “Dk Ulimboka damu yako ilimwagika na
kuamsha ari kwa wananchi kudai huduma bora za afya.” “Dk Ulimboka wewe ni
mpigania haki na afya bora kwa wananchi wote Mungu na watanzania wote tuko
nawe.”
Nae Katibu wa Jumuiya hiyo Dk. Edwin
Chitage alisema kuwa kuwa kurejea kwa Dk. Ulimboka akiwa mzima ni ishara ya
huduma bora aliyoipata akiwa nje ya nchi.
Usiku wa kuamkia Juni 27, 2012 watu
wasiofahamika walimteka, kumpiga, kumng’oa kucha na meno kisha kumtelekeza
kwenye msitu wa pande Dk. Ulimboka.
Wakati amelazwa Hospitali ya taifa
Muhimbili chumba cha wagonjwa mahututi Kitengo cha Mifupa (MOI) alikuwa
akihudumiwa na jopo la madaktari saba akiwapo Profesa Joseph Kahamba.
Licha ya jopo hilo la madaktari
kumhudumia kwa ukaribu lakini walishindwa kupata baadhi ya vipimo ili kubaini
iwapo damu yake ilikua na sumu ama la kwa kusababu baadhi ya dawa zilishindwa
kufanyakazi ndipo uamuzi wa haraka wa kumpeleka nje ya nchi ukafikiwa na
wanachi kumchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 40 za matibabu yake.
Aidha Katibu wa Jumuia ya madaktari Dk.
Chitage amewaahidi wanahabari kuitisha mkutano mapema ili kujuza umma wa
watanzania na dunia kwa kina kuhusu kupona Dk. Ulimboka.
No comments:
Post a Comment