Mhashamu Paschal Kikoti amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwenye
Hospitali ya Bugando. Mungu apokee roho yake mahali pema peponi, Amina.
KANISA
Katoliki Jimbo la Mpanda, limepata pigo la kumpoteza askofu wake wa kwanza,
Paschal William Kikoti (55), aliyefariki dunia kutokana na ugonjwa wa shinikizo
la damu katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Taarifa
za kifo kicho zilitolewa kwa waumini jana usiku katika Kanisa Kuu la kiaskofu
na Makamu Askofu wa jimbo hilo, Padre Patrick Kasomo.
Alisema
kuwa Askofu Kikoti alipatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu Jumapili iliyopita,
majira ya saa moja asubuhi wakati akioga bafuni, na ndipo alipoanguka ghafla
kisha kupoteza fahamu.
Padre
Kasomo alifafanua kuwa, Askofu Kikoti aligunguliwa baadaye na mapadri na
masista walipokuwa wametoka kwenye ibada ya misa ya kwanza saa 2:30 asubuhi
huku akiwa ajitambui.
“Baraza
la Maaskofu lilitafuta usafiri wa ndege siku hiyo, ambayo ilimsafirisha hadi
mkoani Mwanza na kupelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando
kwa ajili ya matibabu hadi hapo janasaa 2:30 jioni alipofariki dunia,” alisema.
Taarifa
hiyo ya Padre Kasomo, iliwashtua waumini wengi ambapo baadhi yao walishindwa
kujizuia na kujikuta wakiangua vilio na wengine kuzirai.
Askofu
Kikoti alizaliwa mkoani Iringa katika Parokia ya Nyabula mwaka 1957 na kupewa
daraja la upadre Juni 29, 1988 humo humo mkoani Iringa.
Mnamo
Januari 14, 2001 Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, aliliunda jimbo jipya la
Mpanda na kumteua Kikoti kuwa askofu wa kwanza kuliongoza.
Kuhusu
mazishi, Padre Kasomo alisema kuwa mwili wa marehemu Askofu Kikoti utawasili
jimboni humo kwa ndege leo ukitokea Mwanza na unatarajiwa kuzikwa rasmi
Jumamosi katika Kanisa Kuu la Kiaskofu Mpanda.
No comments:
Post a Comment