To Chat with me click here

Thursday, August 30, 2012

BABA LEVO, SUMA LEE WAPATA AJALI WAKIELEKEA KIGOMA.


Mchana wa jana Msanii wa bongo fleva Linex aliongea live kwenye Power Jams Ya East Africa Radio na Sam Misago kuhusu ajali walioipata wakielekea kigoma jana. Linex amesema hawakuwa kwenye mwendo wa kasi  kwani show zao ni weekend hivyo mwendo wao ulikuwa mdogo sana na ndio maana haikuwa ajali kubwa .

Dancer mmoja wa Suma lee ameumia Mguu na Gari ya Suma Lee ndio Imeumia sana upande wa mbele, taa zimevunjika. Ajali imesababishwa na basi la abiria lililokuwa katikati ya barabara kwenye kona, ili kulikwepa lazima Suma atoke njee ya barabara na kurudi hapo ndipo gari ikamshinda na kugonga mti.

Linex, Baba levo na Suma lee wana show tatu weekend hii Ijumaa ni Kigoma, Jumamosi ni Kasulu na Jumapili ni Bujumbura. Thanks God wote wako powa.

No comments:

Post a Comment