Baadhi ya Maofisa kutoka taasisi ya HakiElimu
Kutoka kushoto ni
Meneja Kitengo cha Habari wa HakiElimu, Nyanda Shuli, Mhadhiri Adolf Mkenda
kutoka Idara ya Uchumi ya UDSM Mhadhiri wa UDSM, Dk. Kitila Mkumbo
TAASISI
ya HakiElimu leo jijini Dar es Salaam imewakutanisha baadhi ya wahadhiri wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), walimu pamoja na wadau mbalimbali wa elimu
ambapo waliishuhudia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu
ikiwasilishwa ‘live’ mjini bungeni mjini Dodoma kabla ya kutoa maoni yao.
Wadau hao
wa elimu kwa pamoja waliishuhudia kupitia king’amuzi bajeti ya Wizara ta Elimu
na Mafunzo ya Ufundi ikiwasilishwa ‘live’ wakiwa kwenye mkutano kisha baadaye
kutoa maoni yao jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa
kuwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2012/13, Mhadhiri wa UDSM, Dk.
Kitila Mkumbo alisema ameshangaa bajeti hiyo kutouona mgomo wa walimu wa juzi
pamoja na migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ni tatizo kwa elimu na
kuiingiza kama changamoto.
“Binafsi
kati ya vitu ambavyo vimenishangaza ni bajeti hiyo kutotaja mgomo wa walimu
katika bajeti iliyopita kuwa ni miongoni mwa changamoto za wizara hiyo…na hata
migomo ya vyuo vikuu,” alisema Dk. Mkumbo alipokuwa akijadili katika mkutano
huo.
Alisema
wizara imetaja kufanya vizuri katika elimu upande wa msingi na sekondari kwa
kidato, lakini imekwepa kutoa mafanikio kwa kidato cha tano na sita eneo ambalo
limefanya vibaya kwa matokeo ya hivi karibuni. Alikosoa kiwango cha uwiano kati
ya wanafunzi na walimu kilichotatolewa kwa sasa (1:46) kwani idadi kubwa ya
walimu wapo shule za mjini huku hali mbaya ikiwa vijijini.
Aidha
aliongeza kuwa wizara pia imeshindwa kuona migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu ya
mara kwa mara ni changamoto hivyo kushindwa kueleza katika bajeti yake.
“…karibu asilimia 80 ya migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu imesababishwa na Bodi
ya Mikopo ya Elimu ya Juu, lakini hili halikutajwa katika bajeti ya waziri,”
alisema msomi huyo.
Kwa
upande wake Mhadhiri Adolf Mkenda kutoka Idara ya Uchumi ya UDSM akizungumza
katika mkutano huo alisema bajeti iliyowasilishwa ni ya kawaida hivyo ni vigumu
kumaliza changamoto lukuki za elimu zinazoikabili wizara hiyo.
Alisema
bajeti imejivunia ongezeko la idadi ya vyuo vikuu lakini imeshindwa kuonesha
ubora wa vyuo hivyo jambo ambalo ni hatari endapo litaachwa, bila udhibiti.
“…Twaweza kuwa na vyuo vingi lakini suala la ubora ni tatizo lingine. Pia
uandikishaji wa idadi kubwa ya wanafunzi unatakiwa kulinganishwa na
waliokusudiwa kuandikishwa…maana twaweza jivunia kiwango kinapanda kumbe
tunadanganywa na ongezeko la idadi ya watu,” alisema msomi huyo.
Akizungumza
kwenye mjadala Meneja wa Kitengo cha Habari wa HakiElimu, Nyanda Shuli alisema
Serikali haiwezi kufanikisha elimu bora bila kuaandaa walimu bora katika utoaji
wa elimu husika. “Huwezi kutegemea elimu bora pasipo na walimu bora, binafsi
sijaona mkakati wowote mahususi wa kuboresha elimu,” alisema Shuli.
Ameishauri
wizara ya elimu kujiandaa vizuri kimipango kabla ya kutekeleza mpango wa kuwa
na shule ya kidato cha tano na sita kwa kila tarafa ili kuepuka madudu
yaliojitokeza katika mpango wa uanzishwaji shule za kata.
Hata
hivyo kabla ya kuishuhudia bajeti hiyo ikiwasilishwa Dk. Mkumbo na Mkenda
wakiongozwa na mhadhiri mwenzao kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na
Mawasiliano, Ayoub Rioba waliwasilisha mada zilizokuwa zikiiangalia elimu ya
Tanzania na majaliwa yake.
Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Elimu tayari imewasilisha makadirio ya mapato na matumizi
kwa mwaka 2012/13 ambapo jumla ya sh. 724,471,937,000 ili zitumike kuiwezesha
Wizara kutekeleza majukumu yake. Huku sh. 18,561,689,000 zikiwa ni fedha za
ndani na sh. 74,019,627,000 kutoka kwa washirika wa maendeleo.
No comments:
Post a Comment