Wanasayansi wanaoendesha utafiti kuhusu
virusi vinavyosababisha ugonga wa Ebola, wameiambia BBC kuwa, chanjo inayoweza
kutumiwa kuzuia maambukizi ya virusi hivyo huenda isifumbuliwe.
Wiki
chahche zilizopita idara ya ulinzi ya Marekani, Pentagon, ilisitisha ufadhili
wake kwa kampuni mbili ambazo zilikuwa zikiendesha utafiti huo.
Mmoja
wa wataalamu katika jopo hilo amesema kuna uwezekano mkubwa wa chanjo hiyo
itakayotumiwa kuzuia mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola haitatumika.
Ugonjwa
wa Ebola umetajwa kama moja ya magonjwa hatari na ya kuogofya zaidi
ulimwenguni. Virusi
hivyo vinasababisha homa kali ambayo hufanya mtu kuvuja damu katika viungo vya
ndani na hata kupitia sehemu zingine kama vile masikio, mapua na hata ngozi.
Wataalamu
wanasema virusi hivyo ambavyo hushambulia chembe chembe nyeupe na mishipa ya
damu na kusababisha mwasho wa ngozi, macho mekundu, kutapika na mauimivu ya
viungo.
Katika
miezi ya hivi karibuni watu 16, waliaga dunia Magharibi mwa Uganda, kutokana na
ugonjwa huo. Kufikia
sasa hakuna tiba kamili ya ugonjwa huo ambao unaweza kusababisha vifo kwa
asilimia 90 ya watu walioambukizwa virusi hivyo.
Mikakati
ya kujaribu kufumbua chanjo ya kutibu na kuzuia virusi vya Ebola imefadhiliwa
na Idara ya Ulinzi na Taasisi ya Kitaifa ya Afya nchini Marekani NIH. Idara
hizo mbili zimewekeza mamilioni ya dola kwa utafiti huku zikiwa na wasi wasi
kuwa virusi hivyo vinaweza kutumiwa kama silaha za kibiolojia.
Kutokana
na ufadhili huo, chanjo kadhaa zimefumbuliwa na tayari zimefanyiwa majaribio
kwa wanyama na matokeo yake yamekuwa ya kuridhisha.
Kampuni
mbili Sarepta na Tekmira tayari zimeanzisha majaribio ya tiba hiyo kwa
binadamu.
Lakini
kampuni hizo zimefahamaishwa na Idara ya Ulinzi ya Marekani kusitisha utafiti
huo mwa muda kutokana na ukosefu wa fedha. Uamuzi wa mwisho kuhusu ikiwa ufadhili huo utarejelewa tena utatolewa mwezi
ujao.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment