ADAI ASINGEWEZA KUKATAA MAAGIZO
YAO
Waziri wa zamani Fedha, Basil Mramba (Kushoto), Waziri wa zamani wa
Nishati, Daniel Yona (Katikati) na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha, Grey Mgonja wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jana, wakisubiri kuendelea kwa kesi yao ambapo wote wanatuhumiwa
kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh11.7 Bilioni wakati wa
uongozi wao.
ALIYEKUWA Waziri wa
Fedha Basil Mramba, jana aliendelea kumkandamiza aliyekuwa bosi wake na Rais wa
Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akimhusisha moja kwa moja na kutolewa kwa
msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers.
Mramba aliyaeleza hayo jana wakati akijitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili za matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni na kwamba alitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo ili kutekeleza matakwa ya mkataba.

Alidai kuwa kifungu
cha 4.3.1 kilichopo kwenye mkataba huo ulioingiwa kati ya Benki Kuu
ya Tanzania (BoT) na Alex Stewart Government Business Assayers kinasema malipo
yoyote yatakayolipwa na mkataba huo hayatotozwa kodi.
“Mimi nilichofanya ni
kutekeleza matakwa ya mkataba huu kwa sababu Waziri wa Fedha pekee
ndiye mwenye mamlaka ya kutekeleza mkataba huo,” alidai Mramba.
Mramba alikiri kuruhusu
gavana wa BoT kuilipa kampuni ya Alex Stewart, Dola za Marekani 1 milioni
kama malipo ya awali, kwa ajili ya kufanya maandalizi ya ukaguzi wa migodi ya
madini, na kwamba fedha nyingine zingelipwa kwa awamu.
Mramba alisema
aliruhusu malipo hayo kufanyika kutokana na kuwapo kwa barua ya Mei 13,
2003, kutoka kwa Katibu Mkuu wa Rais, Patrick Mombo kwenda kwa Katibu
Mkuu wa Nishati na Madini kuhusu mkaguzi wa dhahabu ikisema “Rais amekubali
Waziri wa Fedha na BoT watafute njia ya kuilipa kampuni ya Alex Stewart
Government Business Assayers”.
“Maagizo yote mimi
niliyachukulia kama ni ya Rais, alikuwa akiagiza watendaji wake
kutekeleza majukumu yote,”alisema Mramba na kuongeza kuwa kwa kuzingatia
makubaliano hayo alitafuta fedha hizo kupitia bungeni katika Bajeti ya Serikali
ya 2003/04.
Kuhusu mkataba,
Mramba alisema kuwa anachofahamu yeye sheria ya BoT inampa mamlaka Gavana
kuingia mikataba na kuisaini na kwamba mikataba yote aliyoingia na watu wengine
ni lazima kodi isamehewe.
Mramba aliiambia mahakama hiyo kuwa, kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers ilikuwa ikitaka malipo bila kodi na kwamba, wao walikubali kutomtoza kodi kutokana na ushauri kutoka kwa wataalamu akiwamo gavana kuwa wamsamehe kodi vinginevyo wangemlipa zaidi.
Hata hivyo, alisema mkataba baina ya BoT na kampuni hiyo haukuwahi kupitia katika kikao cha Baraza la Mawaziri. “Sikudhani kama angeweza kutiliana nao saini kwenye mkataba huo, bila Baraza la Mawaziri kuridhia,”alisema Mramba.
Ushauri
wa TRA
Mramba alibainisha kuwa
Bethar Soka ambaye alikuwa kwenye kamati iliyofanya mchakato wa kuitafuta
kampuni hiyo ya ukaguzi wa dhahabu, aliomba kupata kauli ya TRA kama
kampuni ya Alex Stewart Government Bussines Assayers isamehewe kodi ama la, Mei
26, 2003.
Alidai kuwa baada ya Soka kupeleka ombi hilo Mei 26, 2003, TRA katika majibu yao ya Juni 24, 2003 walisema kuwa hawapendekezi mkaguzi huyo wa dhahabu asamehewe kodi na kwamba barua hiyo ilipelekwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha wakati BoT na kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers iliingia mkataba Juni 14, 2003.
“Inaonyesha barua hiyo ya TRA ilichelewa kwa siku 10, baada ya mkataba kusainiwa, hata hivyo, ushauri huu wa TRA hatukuuhitaji hata kama ungekuja haungekuwa na manufaa,” aliongeza kudai Mramba.
Baada ya maelezo hayo, mmoja wa wanaosikiliza kesi hiyo, Hakimu Saul Kinemela, alimuuliza Mramba, Wizara ya Fedha iliomba ushauri huo TRA wa kazi gani?

Akijibu swali hilo,
Mramba alisema, "Siyo Wizara ya Fedha iliomba ushauri TRA, bali Soka aliomba
ushauri huo kama mwanakamati iliyokuwa ikifanya mchakato wa kutafuta kampuni
hiyo na kwamba Soka yeye alikuwa ni mtumishi wa wizara yake.
Alibainisha
kuwa Soka asingeweza kumshauri Waziri, anayeweza
kumshauri ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu.
Mbali na Mramba, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.
Mbali na Mramba, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.
Jaji John Utamwa
aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12, mwaka huu itakapoendelea na utetezi.
Utetezi
wa awali
Mramba (71) alianza
kujitetea, Agosti 22, mwaka huu ambapo alidai kuwa Serikali iliiteua BoT
ifanye kazi ya kutafuta kampuni inayoweza kufanya kazi hiyo hivyo
ikaingia mkataba na kampuni iliyochaguliwa ya Alex Stewart Government
Bussines Assayers.
Waziri huyo wa zamani
aliongeza kudai kuwa aliyeagiza BOT kufanya kazi hiyo ya kumtafuta mkaguzi wa
dhahabu ni Rais wa Awamu ya Tatu, Mkapa na kwamba wakati huo yeye akiwa Waziri
wa Wizara ya Fedha alipewa jukumu la kuhakikisha gharama za kumlipa mkaguzi
huyo zinapatikana ndani ya Serikali au BoT ama pengine popote.
Alifafanua kuwa kati
yake yeye na gavana hakuna aliyekuwa na mamlaka juu ya mwingine na
kwamba gavana alikuwa na wajibu wa kufanya mchakato wa kumtafuta mkaguzi
wa dhahabu.
Mramba alisisitiza
kudai kuwa yeye hakuhusika kwenye mchakato huo kwa kumtafuta wala kumleta hapa
nchini wala kumtuma mwakilishi yeyote kumwakilisha kwenye
kamati iliyoteuliwa kufanya mchakato huo bali alipewa agizo la kumlipa.
“Mimi kama waziri
sikuwa na mtu wangu kwenye ile kamati, lakini Wizara ilituma mwakilishi, ambaye
alikuwa mwanasheria Bethar Soka wakati wa kuhoji kampuni mbili ili
wachague na kwenye kujadili vipengele vya mkataba,”alisema.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao waliipatia msamaha wa kodi isivyo halali, Kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment