Theopista F. N. Sanga |
Ilikuwa siku kama ya
leo miaka tisa (9) iliyopita katika kanisa la Mt. Joseph, jimbo kuu la
Dar-es-Salaam, ambapo mpendwa wetu Theopista F. Nsanzugwanko na Ndg. Deus Sanga
walifunga ndoa.
Kama kila mmoja wetu
afahamuvyo juu ya maisha ya ndoa hujawa na misukosuko mingi ya kimaisha,
majaribu, shida za kiuchumi na makandokando mengi, halikadharika ndoa ya
Theopista nayo haikukoswa na magumu hayo ya kimaisha.
Lakini kwakuwa
Theopista Nsanzugwanko, alilelewa katika familia ya kikristo ambayo mkuu wa
familia hiyo Hayati Baba Firdbety Nsanzugwanko (Mungu amlaze mahali pema peponi)
alikuwa ni mtumishi mwema wa Mungu, hakusita kuwaongoza watoto wake akiwemo
yeye (Theo) katika misingi mizuri ya kidini, akiwafundisha kuwa WAVUMILIVU,
WANYEYEKEVU, WENYE KUELEWA WENGINE na WENYE KUMWAMINI NA KUMCHA MUNGU.
Kutokana na
mafundisho hayo mema ya mzee wao, ndugu yetu Theo ameweza kuvumilia mengi mno
katika kipindi hicho chote cha maisha yake ya ndoa. Hivi sasa Mungu amembariki
na watoto wawili Witness Sanga (Mke) na Winston Sanga (Mme). Pia katika
majaribu na magumu yote, mama huyu wa watoto wawili ameweza kumudu kuwasomesha
watoto wake wote wawili, yeye mwenyewe kujiendeleza, pia kusimamia mambo muhimu
ya kuimarisha familia yao kama ujenzi wa nyumba na mengine mengi, kwa msaada
mkubwa wa mumewe ndg. Deus Sanga pamoja na Mungu akiwaongoza.
Siri kubwa ya
mafanikio ya Theo katika ndoa yake, ni uchaji na uvumilivu alionao, ambao
wanawake wengi na wadada wa kileo wamekuwa hawana sifa hii ya uvumilivu. Ni vyema
wanawake wakaiga tabia hii ya Theopista na kujiepusha na tamaa za kupata
maendeleo ya haraka haraka ambazo huweza kuharibu maisha yao ya ndoa.
Katika kusherehekea
siku hii kubwa ya ndoa yake, Theopista ameandika haya kwenye kurasa zake za
facebook kwa marafiki zake;
“mungu ni mwema ukimtumaini sina neno kubwa la kumshukuru bali nikusema aksante kwa upendo wake kwa familia hii,friends leo ni annivesary ya ndoa yetu mm na my lovely husband Deus Sanga kwani siku kama ya leo miaka kenda iliyopita tulifunga ndoa katika kanisa la mt joseph dsm na tunamshukuru mungu kwa zawadi ya Witness na Winston ehee mungu naomba endelea kupigania ndoa hii upendo na amani vitawale siku zote”
Kwakweli, Maxmillian Kattikiro Blog, inapenda kumpongeza sana Theopista kwa mafanikio ambayo
ameyapata na pia tunamwombea kwa Mungu azidi kumbariki na kumpitisha salama
kwenye njia zake na hivyo siku moja aweze kufanya anniversary ya miaka 100 ya
ndoa yake.
Happy Anniversary
Theopista & Deus Sanga.
No comments:
Post a Comment