Kwa kuwa
mchakato wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote wanaotaka
kushiriki katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya
83 ambazo zote zinapatikana katika tovuti ya Tume ambayo ni
www.katiba.go.tz
Kusoma Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba ya sasa ubora na
upungufu wake na kuelewa utaratibu na masharti yanayoainishwa kisheria
kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.1.
1. MAMBO
YA KUZINGATIA
Kwa kuwa
uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa na kusimamiwa na Sheria, Tume
inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:
2.
(a)Nani Mwenye Haki ya Kushiriki:
Mtu
yeyote ambaye ni Mtanzania kwa uraia wake anayo haki ya kushiriki katika
mchakato huu. Mtu ambaye kwa asili yake ni Mtanzania, lakini amepoteza uraia wa
Tanzania hatoweza kushiriki; na akifanya hivyo atakuwa ametenda kosa chini ya
Sheria.
(b)Utaratibu
wa Utoaji Maoni: Njia tatu za ukusanyaji wa maoni zitatumika.
3. Njia
hizo ni kama zifuatazo:
4. (i)
Utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti www.katiba.go.tz
barua pepe ya Tume, katibu@katiba.go.tz (This e-mail address
is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ),
nukushi + 255-22-2133442 na +255-224-2230769
(ii)Utoaji
wa maoni kupitia nyaraka na barua zitakazotumwa kwa Tume kutumia anwani ya
Tume, ambao ni: Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681 DSM au Ofisi
ndogo ya Tume, S.L.P. 2775 Zanzibar.
Endapo
Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania wakati wa ukusanyaji
wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama Watanzania wengine walioko
nchini kwa kuhudhuria mikutano ya kukusanya maoni iliyoandaliwa na Tume.
5. (iii)
Utambulisho wa Mtoa Maoni: Kila mtu atakayetoa maoni yake Tume anapaswa
kubainisha mambo yafuatayo:-
(i)
majina yake matatu;
(ii) namba
ya pasi yake ya kusafiria na mahali ilipotolewa;
(iii) nchi
na mji anaoishi;
(iv) endapo
atatumia nyaraka au barua, ataambatanisha kivuli cha pasi yake (ukurasa
unaoonyesha maelezo ya mtu mwenye pasi hiyo).
No comments:
Post a Comment