Moja
ya sababu kubwa inayochangia kurudisha nyuma maendeleo yetu, ni kwa watawala
kudharau elimu na walimu wetu. Katika nchi hii, profession yoyote si kitu mbele
ya mwanasiasa. katika nchi zilizoendelea, ukimuuliza mtoto unataka kuwa nani?
Atakujibu kuwa anataka kuja kuwa mwalimu.
Wenzetu waalimu ni watu wa muhimu sana katika makuzi na kuelimisha jamii. Watoto, wazazi na hata serikali wanawapa heshima yao. Pia walimu wanamaslahi mazuri yanayowapa motisha, na mara nyingi wazazi huwa wanawapa hata zawadi waalimu wanaopendwa na watoto wao na kuona jinsi wanavyowaelimisha wototo wao.
Hapa kwetu miaka ya zamani ilikuwa hivyo, nakumbuka kijijini kwetu walimu, wauguzi na viongozi waliheshimika sana. Waalimu walikuwa wanasikilizwa na walikuwa wakishauri jamii mambo mbalimbali. Ila bado hadi leo ushawishi wao ni mkubwa hasa huko vijijini.
Sasa hawa wanasiasa wanaowabeza leo, wasishangae wakiona waalimu wakileta mapinduzi kwa kuwaambia wananchi hasa vijijini kuwa serikali yao haina nia njema ya kuwaletea maendeleo na kuwaelekeza cha kufanya ili kuiondoa madarakani. Mara nyingi sisi hasa waafrika tumekuwa na ulevi wa madaraka na kuamini mambo yasiyo halisi.
Inashangaza kuona kuwa, badala ya serikali kushughulikia matatizo husika, wenyewe wanataka kujiambinisha kuwa waalimu wanatumika kisiasa. Hivi kweli mtu akidai haki yake aliyoikosa miaka zaidi ya kumi, vilevile akiwa kwenye lindi la matatizo ya kupambana na maisha kwa ugumu wake. Leo unakuja kumwambia yeye si kitu na anatumika?
Bila ya hawa waalimu tusingekuwa na Madaktari, Maengineer, Wanasheria, wahasibu, wachumi, na wataalamu wengine wote. Huyu Mzee atakuwa ameongeza hasira ya waalimu dhidi ya serikali. Walifanikiwa kupandikiza chuki kwa madaktari dhidi ya wananchi, ila kwa hili la waalimu ni budi serikali ibadili namna ya kumaliza mgogoro huu uliodumu kwa muda mrefu sana.
No comments:
Post a Comment