Ili
kufikia malengo yetu ya kuzunguka kwenye Miji mbalimbali ya UK kuhamasisha
Watanzania waishio uk kujiunga na Chadema, kueneza kampeni ya m4c
na kufungua matawi mengine, Tawi la Chadema London linapenda
kuwatangazia Watanzania wote waishio katika Mji wa Reading na maeneo ya jirani
kuwa kutakuwa na mkutano mkubwa wa M4C UK utakao fanyika Tarehe 26/08/2012
siku ya Bank holiday.
Dhumuni la
mkutano huo ni kuwahamasisha Watanzania waishio UK kujiunga na chama, kushiriki
katika harakati za mabadiliko, kusajili wanachama wapya,
kuchagua wawakilishi wa muda kutoka mji wa Reading pamoja na kuanzisha
mfuko wa kufa na kuzikana kwa manufaa ya watanzania wote.
Tumekusudia
kuanzisha Mfuko wa kufa na kuzikana kwa sababu mpaka hivi sasa Mtanzania akifariki
akiwa UK hakuna taasisi wala ofisi yoyote inayotoa msaada. Jukumu
ambalo kwa muda mrefu Serikali yetu kupitia ubalozi umelipuuzia na kushindwa
kulisimamia na kulishughulikia.
Mfuko huu utasaidia katika kumsafirisha Marahemu na Mfiwa pamoja na kusaidia kushughulikia matatizo na usumbufu utakaojitokeza baada ya mtu kufariki dunia na kusaidia matatizo mbalimbali yakiwemo majanga ya dharura.
Mfuko huu utasaidia katika kumsafirisha Marahemu na Mfiwa pamoja na kusaidia kushughulikia matatizo na usumbufu utakaojitokeza baada ya mtu kufariki dunia na kusaidia matatizo mbalimbali yakiwemo majanga ya dharura.
Pia
katika mkutano huo wanachama mbalimbali wa CCM walio na uchungu na nchi yetu na
wanaopenda maendeleo na mabadiliko ya kweli watapewa nafasi ya kujiunga
na Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama sehemu moja wapo
ya kampeni yetu ya Kuvua Gamba na Kuvaa Gwanda ukiwa
Ughaibuni.
Mkutano utafanyika siku ya
Tarehe 26/08/2012, Kuanzia saa saba mchana mpaka saa
kumi na mbii jioni.
Risc Reading International
Solidarity Centre,
35-39 London Street,
Reading, RG1 4PS
Watanzania
wote, marafiki na wadau mbali mbali wa maendeleo na mabadiliko ya kweli
mnakaribishwa sana.
Huu ndio
wakati wa mabadiliko, kusimama na kusema tumechoka!
KWA
MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA;
MWENYEKITI: Chris Lukosi 07903828119,
MWENYEKITI: Chris Lukosi 07903828119,
KATIBU
MWENEZI: Chris Chagula 07405889880
au
Tutumie email kupitia chademauk@gmail.com
au
Tutumie email kupitia chademauk@gmail.com
No comments:
Post a Comment